Makamu mwenyekiti wa Baraza la Vijana Taifa JULIANA SHONZA ameanza kwa kishindo ziara yake Mkoani mbeya moja kwa moja akijikita Vijijini kwa lengo la Kujenga na kuimarisha chama chake.
Ziara yake ilianza jana kwenye kata ya MSIA ambapo katika kata hiyo alifanya mkutano wa hadhara uliokua na mamia ya watu.katika mkutano huo,Juliana Shonza alijikita katika kueleza namna wwananchi wanavyotakiwa kujitokeza kwenye sensa inayoanza agousti 26 mwaka huu,pia alielezea umuhimu wa wanachi kujitokeza katika kutoa maoni ya katiba mpya kwa manufaa ya taifa hili na wananchi wake
Sehemu kubwa pia ya mazungumzo yake kwa wananchi alijikita kwenye umuhimu wa vijana na wanawake kuijiingiza kwenye siasa bila kuogopa mabavu na vitisho toka chama Tawala.Pia alizungumzia namna wanachi wanavyoibiwa zao lao la kahawa na viongozi wa serikali ya ccm pamoja na makampuni binafsi.
Leo Makamu mwenyekiti huyo atakuwa na mkutano wa hadhara katika kata ya ITAKA amabapo anategemea kukutana na wananchi wa kata hiyo.
Katika ziara hiyo makamu mwenyekiti ameshirikiana vyema na viongozi wa jimbo,viongozi wa baraza la vijana mkoa wa mbeya ambao kwa umoja wao wamekuwa wakishirikiana kwa ukaribu katika ziara hii
Ziara hiyo itaendelea kesho kwenye kata ya IYULA na kwa muda wa wiki moja ijayo atajikita kwenye wilaya la MBARALI
Ikumbukwe wazi Makamu mwenyekiti anajitolea kufanya ziara hii,anasisitiza vijana kuendelea kujitolea kwenye ujenzi wa chama.Pia mwenyekiti huyo huyo amepitisha bakuri la kuchangia ziara yake hiyo kwa wadau mbalimbali, wa mkoa wa mbeya na wale wanaokiunga mkono chadema,hatimaye amefanikiwa kuanza ziara hiyo inayoonekana kuwa na mafanikio makubwa kutokana na idadi ya watu wanaohamia chadema na kuomba kadiza chama hicho,Pia wingi wa wafuasi wa chadema kwenye mikutano hii ni wazi kwamba CHADEMA inakubarika mkoani mbeya na vijiji vyake.
No comments:
Post a Comment