Migomo, maandamano na vurugu zinazofanywa na vijana katika maeneo mbalimbali nchini zinaweza kuepukika kama baadhi ya viongozi wa Serikalini watatekeleza kwa vitendo sera ya taifa ya maendeleo vijana ya mwaka 2007.
Hayo yalisemwa jana na Katibu wa Asasi isiyo ya Kiserikali ya Amani The Foundation of Life ya mkoani Mbeya, Philimon Mwansasu wakati akizungumza kwenye mdaharo wa Jukwaa la vijana wilayani Kyela.
Mwansasu alisema kuwa Sera ya Taifa ya maendeleo ya vijana haitekelezwi ipasavyo na viongozi Serikalini kutokana na baadhi yao kutoielewa ipasavyo na wengine kwa uzembe wa makusudi.
Alisema kwa mujibu wa Sera hiyo ambayo ilianzishwa mwaka 1995 na kubadilishwa mwaka 2007, viongozi wa Serikali wanatakiwa kuanzisha umoja wa vijana kwenye maeneo yao na kuwasimamia.
Mwansasu alisema kuwa sera hiyo inaelekeza kuwa Mkuu wa Mkoa ndiye anayestahili kuwa Mwenyekiti wa vijana wa Mkoa, Mkuu wa Wilaya anapaswa kuwa Mwenyekiti wa umoja wa vijana wa wilaya yake, Diwani anastahili kuwa Mwenyekiti wa vijana kwenye kata na Mwenyekiti wa Kijiji naye anapaswa kuongoza vijana kwenye eneo lake.
Alisema kwa hali ilivyo hivi sasa viongozi hao wametelekeza majukumu yao, hali inayosababisha vijana kukosa umoja na punde wanapona hawatendewi haki huamua kujiongoza wenyewe kwa kufanya mambo yasiyostahili kama vile migomo, vurugu au maandamano.
“Wakati mwingine tunawalaumu vijana kwa kufanya migomo, maandamano na vurugu bila kufikiria chanzo cha tatizo, nadhani viongozi hawa wasiotekeleza wajibu wao kwa vijana ndio wanaopaswa kulaumiwa kwa kutotekeleza wajibu wao,” alisema Mwansasu.
Alisema kuwa Sera ya maeneleo ya vijana inaelekeza kuwa kila halmashauri nchini itenge asilimia kumi ya pato lake kwa ajili ya maendeleo ya vijana, lakini katika halmashauri nyingi fedha hizo hawapewi vijana na badala yake huelekezwa kwenye mambo mengine.
Alisema kuwa kama vijana wataungana na kuunda chombo chao, watakuwa na sauti ya kuziomba fedha hizo na kuzitumia kwenye vikundi vyao kwa ajili ya kujiletea maendeleo.
Mwansasu aliwataka vijana hao kuhakikisha wanasajili Jukwaa lao la vijana ili waweze kuwa na uhalali wa kisheria wa kuomba fedha hizo ili wakopeshwe na kuzitumia kwa shughuli za maendeleo ya vijana.
“Hakikisheni kuwa mnasajili hili Jukwaa la vijana, kwani mkishasajili mtakuwa na uwezo wa kuwawajibisha viongozi wenu na pia kuomba hizi fedha zinazotengwa kila mwaka kwa ajili ya vijana ili mzitumie kukopeshana kwenye vikundi vyenu na kujiletea maendeleo,” alisema Mwansasu.
Katika mdahalo huo, vijana wapatao 80 wanaounda Jukwaa la Vijana la Wilaya ya Kyela walichanga jumla ya shilingi 400,000 kwa ajili ya kuwawezesha wawakilishi wao kwenda Jijini Dar es Salaam kusajili jukwa hilo ili litambulike rasmi kisheria.
CHANZO: NIPASHE

No comments:
Post a Comment