Tawi la
Chadema Washington DC limepata Viongozi wapya walioshika nafasi za waliokuwa
Viongozi wa muda. Katika Uchaguzi huo Cosmas
Wambura amechaguliwa kuwa Mwenyekiti mpya kuchukua nafasi ya aliyekuwa
Mwenyekiti wa Muda Kalley Pandukizi.
Nafasi ya Katibu imechukuliwa na Isidori
Lyamuya aliyechukua nafasi ya Liberatus
Mwang’ombe aliyekuwa Katibu. Nafasi ya Mweka hazina imechukuliwa na Ludigo
Mhagama na nafasi ya katibu mwenezi imechukuliwa na Hussein Kauzella. Nafasi
nyingine zilizogombewa ni Wenyeviti na Makatibu wa Mabaraza ya Vijana, Wanawake
na Wazee. Pia kulikuwa na nafasi ya Afisa Habari wa Chama. Akiongea baada ya
Uchaguzi Mwenyekiti aliyechaguliwa ndugu Cosmas Wambura amesema atatoa
ushirikiano mkubwa katika kuendeleza shughuli mbalimbaliza kukijenga Chama. Pia
Katibu mpya amesema watashirikiana na Mwenyekiti na wanachama wengine wote
kuhakikisha Chama kinzidi kuwa Imara na kupata wanachama zaidi.
Mwenyekiti mpya wa Tawi la Chadema washington DC Ndugu Cosmas Wambura akiongea mambo machache baada ya kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti mpya.
Aliyekuwa Mwenyekiti aliyemaliza muda wake Kalley Pandukizi akimkabidhi Kitabu cha Katiba na Sera za Chama Mwenyekiti mpya Ndugu Cosmas Wambura.
Mwenyekiti mpya wa Chadema Washington Cosmas Wambura akipeana mikono ya pongezi na Katibu mpya Ndugu Isidori Lyamuya.
Kutoka kushoto Katibu mpya Isidory Lyamuya, Mwenyekiti mpya Cosmas Wambura, Katibu aliyemaliza muda wake Liberatus Mwang'ombe na Mwenyekiti aliyemaliza muda wake Kalley Pandukizi.
Baadhi ya wanachama wa Chadema walioshiriki zoezi la Uchaguzi la kupata Viongozi wapya wa Chadema Washington DC.
No comments:
Post a Comment