Saturday, June 30, 2012

Serikali: Bil. 14/- zimeokolewa DECI


JIBU LA SWALI LA MBUNGE KAWE
SERIKALI imesema kuwa imefanikiwa kuokoa kiasi cha sh bilioni 14.81 kati ya 39.27 zinazodaiwa na wananchi ambao walikuwa wanachama wa asasi ya panda mbegu uvune mara mbili (DECI).
Naibu Waziri wa Fedha, Janeth Mbene, aliliambia Bunge mjini Dodoma jana wakati akijibu swali la mbunge wa Kawe, Halima Mdee (CHADEMA), akisema kuwa fedha hizo zimezuiliwa katika akauti zinazomilikiwa na wakurugenzi wa DECI katika mabenki mbabalimbali nchini.
Alisema kuwa hatima ya fedha hizo itategemea hukumu ya kesi namba 109/2009 iliyofunguliwa Juni 12, 2009 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.
Mbene alisema kuwa Julai 17 mwaka huu, mahakama itatoa uamuzi kama washtakiwa wana kesi ya kujibu au hapana.
Katika swali lake la msingi, Mdee alitaka kujua ni kiasi gani cha fedha kimeokolewa na serikali iwataje vigogo waliohusika na ubadhirifu huo ulioisababishia hasara.
Alisema kuwa Waziri wa Fedha aliyepita, Mustafa Mkulo, aliwataja vigogo waliohusika na ubadhirifu wa fedha hizo lakini hadi sasa hakuna kinachoendelea.
Mdee pia alitaka kujua ni kwa nini serikali isitoa maelekezo ili fedha hizo ambazo zimekaa kwa muda mrefu ziweze kurudishwa kwa Watanzania ambao waliingia katika hasara hiyo.

Tanzania Daima

No comments:

Post a Comment