Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, alisema jana wakati akijibu hoja za wabunge zilizojadili kwenye hotuba ya bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu na Wizara na Taasisi zake kwa mwaka wa fedha 2012/2013.
Alisema itaanzishwa wakati wowote baada ya maandalizi kukamilika na kwamba utekelezaji wake uko katika hatua nzuri baada ya kamati ndogo iliyoteuliwa na Waziri wa Katiba na Sheria yenye wawakilishi wa Waislamu na Serikali imetoa taarifa yake ya mwanzo ya namna ya kuanzishwa kwa Mahakama ya Kadhi.
Waziri Mkuu alisema mambo yatakayoshughulikiwa na mahakama hiyo ni pamoja na Ndoa na Talaka, Mirathi, Wosia, Hiba/Zawadi/ Tunu, Wakfu; Malezi ya Watoto na Usuluhishi wa Migogoro ya Kiislamu.
Mahakama hiyo haitahusika na Mashauri ya Jinai.
Alisema, “napenda kulijulisha Bunge lako Tukufu kwamba, Kamati Kuu inayojumuisha Viongozi wa Waumini wa Dini ya Kiislamu na Serikali chini ya Uenyekiti wangu, kimsingi imekubaliana kwa kauli moja Uanzishwaji wa Mahakama hiyo Nchini itakayokuwa nje ya Mfumo wa Serikali.” “...upo umuhimu na dhamira ya kweli ya kuanzisha Mahakama ya Kadhi Tanzania Bara aidha, mahakama hiyo itagharamiwa na kuendeshwa na Waumini wa Dini ya Kiislamu wenyewe. Serikali kwa upande wake hususan katika hatua hizi za awali za kuanzishwa kwa Mahakama hii itaendelea kushirikiana kwa karibu ili kuhakikisha kuwa azma hii inafanikiwa.”
Pinda alikuwa akijibu hoja za wabunge waliotaka kufahamu maendeleo ya Mahakama hiyo huku wakitaka Serikali itimize ahadi yake hiyo ambayo ipo katika Ilani ya Uchaguzi ya CCM. Wabunge hao na majimbo yao kwenye mabano ni Hamad Rashid Mohammed (Wawi); Rashid Ali Abdallah (Tumbe); Ahmed Juma Ngwali (Ziwani) na Hussein Nassor Amar ( Nyang’hwale).
Pinda alisema; “Katika kikao cha mwisho cha pamoja kati ya Serikali na ujumbe wa Wawakilishi wa Waumini wa Kiislamu kilichofanyika Machi mwaka huu, tumekubaliana katika kuwezesha suala hilo liende kwa haraka, kwa kuanzia, ni vyema zikaanzishwa Mahakama za Kadhi katika baadhi ya maeneo machache nchini. Lengo ni kuwezesha umma kulielewa vizuri suala hili kinyume na hisia potofu zilizopo sasa zikihusisha Mahakama ya Kadhi na Sharia chini ya Dini ya Kiislamu”.
. Alisema katika kikao cha mwisho cha Kamati Kuu inayosimamia suala hilo iliamuliwa na pande zote kuwa baadhi ya wajumbe kutoka upande Waislamu na Serikali wakafanye ziara ya mafunzo katika nchi za India, Uingereza, Kenya na baadaye Zanzibar ili wakajifunze namna ya kuratibu na kuendesha Mahakama za Kadhi katika nchi hizo ambazo zina Mahakama za Kadhi kwa muda mrefu.
“Lengo ni kupata uzoefu na kujua njia bora ya kutuwezesha kuanzisha Mahakama hiyo nchini. Ziara hiyo inatarajiwa kufanyika hivi karibuni na kugharimiwa na Serikali,” alisema.
Alisema wataalamu wa kuanzisha mahakama hiyo watakwenda nchini Kenya, India, Uingereza na Zanzibar kujifunza jinsi ya kuanzisha chombo hicho na kwamba ziara hiyo itagharamiwa na serikali.
Chanzo - Wavuti
Nadhani mheshimiwa waziri mkuu ameshindwa vibaya kujenga hoja. Anasema mahakama ya kadhi itaendeshwa nje ya mfumo wa serikali, sasa serikali inajihusisha,tena kwa kuharakisha uundwaji wamahakama ya kadhi kwa lengo na sababu zipi? pia serikali inasukumwa na nini kugharimia ziara za kwenda India, kenya, uingereza & zanzibar kujifunza uendeshaji wa mahakama ya kadhi? Mbona ipo wazi kabisa kuwa kuna ajenda ya siri hapa!
ReplyDeletevibaya kujenga hoja. Anasema mahakama ya kadhi itaendeshwa nje ya mfumo wa serikali, sasa serikali inajihusisha,tena kwa kuharakisha uundwaji wamahakama ya kadhi kwa lengo na sababu zipi? pia serikali inasukumwa na nini kugharimia ziara za kwenda India, kenya, uingereza & zanzibar kujifunza uendeshaji wa mahakama ya kadhi? Mbona ipo wazi kabisa kuwa kuna ajenda ya siri hapa!
ReplyDelete