Saturday, June 16, 2012

Nassari afunika nyumbani kwa sioi sumari

Katika Hali isiyokuwa ya kawaida, siku ya Jana mbunge aw arumeru mashariki Mhe. Nassari dogo janja, aliendesha harambee kwa ajili ya ku drill maji, kujenga vyoo na bweni kwenye shule ya mazoezi ya elimu Maalum Patandi iliyoko maeneo ya tengeru kwenye kata ya akheri.

Hii ndio kata anayotokea mbunge aliyetangulia na aliyekuwa mgombea Ubunge wa CCM sioi sumari.

Marehemu sumari aliahidi kuchimba maji kwa miaka na hakuwahi kutekeleza. Leo dogo janja katekeleza akishirikiana na wananchi (participatory development) . Heko kwako dogo janja, kutekeleza ahadi Mpaka nyumbani kwa mpinzani wako.

No comments:

Post a Comment