Mwenyekiti wa Jumuia ya Madaktari nchini, Dk. Steven Ulimboka leo mchana alifikishwa Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Julius Nyerere kwa ajili ya kupelekwa nchini Afrika Kusini kwa matibabu zaidi baada ya madaktari kubaini kuwa ana mtatizo ya kitabibu yanayomkabili likiwemo la mtikisiko wa ubongo.
Mwenyekiti huyo alifikishwa uwanjani hapo majira ya saa 8.30 na ndege aliyosafiri nayo iliondoka saa 10.15. Uwanjani hapo kulikuwa na wanaharakati ambao walikuwa na mabango, kinyume cha matarajio ya wengi walizani kuwa angeteremshwa na kuingizwa na machela Uwanjani hapo lakini gari lililombeba lilipita moja kwa moja hadi ndani ya uwanja huo.

Madaktari wakiwa wamebeba mabango yakiwa na ujumbe mbalimbali kuhusiana na mkasa uliopata Daktari mwenzao Dr Ulimboka wakiwa Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mw Julias Nyerere wakimuaga wakati anapelekwa Afrika Kusini kwa matibabu zaidi.
No comments:
Post a Comment