WANANCHI wa wilaya ya Gairo, mkoani Morogoro, wamependekeza Katiba mpya itamke kuwa mafisadi, waingizaji na wauzaji dawa ya kulevya wapigwe risasi hadharani na Rais ashtakiwe endapo atabainika kushindwa kuwajibika.
Wakitoa mapendekezo hayo kwenye baraza la Katiba lililoandaliwa na asasi ya Kijogoo ikishirikiana na Wataalam Group wa mkoani hapa kwa ufadhili wa Foundation for Civil Society, Emanuel Mgendi, alisema nchi za Afrika zinakabiliwa na viongozi wenye tamaa ya mali na wanatenda watakavyo kwa kuwa hakuna sheria inayowabana.
“Lazima kuwe na kitu kinachotoa hofu kuwajengea uzalendo wa kweli juu ya taifa,” alisema Mgendi.
Anjelina Michael na Stella Mwegoha walitaka Katiba iwape nguvu wananchi katika kuhoji, kudai na kuwaondoa madarakani viongozi wasiowajibika kwa wananchi ili kuongeza nidhamu ya uwajibikaji kwa raia na kuharakisha maendeleo kusudiwa.
“Sasa hivi watu hawafanyi kazi; wanashinda vijiweni, watumishi nao wanafanya watakavyo huku dola nayo ikiyumba kiuadilifu kutokana na kutokuwepo nidhamu ya utumishi kwenye Katiba na hakuna anayeguswa na hali hii kwa kuwa hakuna kitu cha kuwasukuma,” alifafanua Stella.
Pamoja na hayo, walipendekeza muungano wa serikali tatu, ili kuimarisha historia ya Tanganyika.
No comments:
Post a Comment