Saturday, March 9, 2013

Mh Leticia Nyerere azungumzia suala la Uraia wa Nchi Mbili


Mbunge wa viti maalum Mh. Leticia Nyerere amewatoa mashaka Watanzania wote waliokua nje ya nchi juu ya suala la uraia wa nchi mbili.

Akiongea na Wakazi wa DMV Marekani Mheshimiwa  Leticia amesema anazidi kutoa msukumo bungeni na kwa Tume ya  Katiba ili suala la Uraia wa Nchi mbili kuweza kuingizwa katika katiba mpya. Mh Leticia amewahakikishia Watanzania waishio nje ya nchi kuwa  tume itatumia busara zake ili kuingiza kipengele cha uraia wa nchi mbili katika katiba hiyo mpya kwani kufanya hivyo  kutawezesha raia wa Tanzania walioko nje kusaidia katika shughuli mbalimbali za Kiuchumi kwa kuwawezesha kuwekeza mitaji yao na miradi mbali mbali ya kukuza uchumi.

Mh Leticia alitoa mfano wa baadhi ya Nchi kama Kenya ambayo wanatumia utaratibu huu wa wananchi wao kuwa na Uraia wa Nchi mbili jinsi walivyonufaisha nchi yao kiuchumi na wao kunufaika pia.






Chanzo Swahilivilla Blog

No comments:

Post a Comment