Baada ya kikao cha ndani kati ya wajumbe wa Kamati ya Utendaji Wilaya ya Tarime na madiwani, kubaini udhaifu wa kiuongozi ulioruhusu kuzuka kwa makundi yaliyokuwa yakidhoofisha utendaji kazi na uhai wa chama wilayani hapa, Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe amevunja uongozi wa wilaya hiyo (kwa maana ya Kamati ya Utendaji).
Uamuzi huo uliofanyika leo mchana, ulipokelewa kwa mikono miwili na wajumbe wa kikao hicho.
Baada ya kikao hicho cha Kamati ya Utendaji na madiwani wa CHADEMA Wilaya ya Tarime, Mwenyekiti Mbowe alikutana na wanachama na wadau wa chama wa Tarime, kwenye kikao cha ndani, ambapo kwa kauli moja waliupokea kwa furaha uamuzi huo wa kuvunjwa kwa uongozi huo, huku wakiomba nafasi hizo za uongozi zijazwe mapema kwa ajili ya kuendelea kukiimarisha chama.
Uongozi wa chama katika ngazi za kata hadi misingi utaendelea kufanya kazi kama kawaida.
Kwa hatua hiyo, uchaguzi wa kupata uongozi wa Kamati ya Utendaji ya muda, utafanyika ndani ya mwezi mmoja ukisimamiwa na ngazi ya juu
Mwenyekiti Mbowe amewataka watu wa Tarime kutopoteza ari yao ya dhati katika kukisimamia na kukipigania CHADEMA katika kuendesha mapambano ya ukombozi wa pili wa nchi, ambayo ilikuwa ni mfano wa kuigwa wa wanaChadema nchi nzima, kiasi cha watu kusalimiana..."mambo...kama Tarime..."
No comments:
Post a Comment