Monday, March 11, 2013

LISSU ATAKA WAKAZI WA DAR WAJIUNGE KATIKA UKOMBOZI WA NCHI

Akihutubia ktk Mkutano wa Hadhara uliofanyika Maeneo ya TABATA LIWITI Mh. Lissu alionyeshwa kushangazwa na idadi ndogo ya watu waliohudhuria mkutano wakati maanadalizi yalikuwa ya muda mrefu," inashangaza kwa mji mdogo kama ITIGI mkutano umeitishwa asubuhi tu kwa matangazo ya mtaani kufikia mchana tunaanza mkutano idadi ya watu ni zaidi ya mara 3 ya nyinyi, tena nyinyi mpo katikati ya jiji, kule singida hakuna magazeti wala TV lakini watu wanamwamko wa mageuzi kuliko Dar" alishangaa.


Alisema mageuzi yoyote ya kiuongozi Duniani huwa yanaanzia mijini Tusijidanganye."Tatizo watu wa Dar hamfanyi kazi ya siasa,  Dar inarudisha nyuma harakati za kisisasa ktk nchi hii" mnaishia kusema tumeibiwa kura mbona ubungo hawakuiba au kawe, hayo ni majibu mepesi kwenye swali gumu, lindeni kura sheria inasema kaa mita 300 kutoka kituo cha kupigia kura alisema"

mikoa kama Shinyanga , Kigoma, Arusha, Mwanza, Kilimanjaro ipo juu ktk harakati za kuikomboa nchi hii lakini Dar ni ya mwisho.
Bila wakazi wa Dar kubadilika na kuwa mstari wa mbele katika harakati za mageuzi ukombozi wa nchi hii unaweza chukua muda mrefu sana ingawa kwa sasa dalili za anguko la mfumo uliopo zipo dhahiri kabisa alisema. 

No comments:

Post a Comment