Chama cha Demokrasia na maendeleo (Chadema) wilaya ya chato mkoa wa geita, kimeanza mikakati ya kumuondoa kwenye wadhifa wake mbunge wa jimbo la Chato ambaye pia ni Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli katika uchaguzi mkuu ujao mwaka 2015.
Mikakati hiyo inatarajiwa kuanza mapema mwaka huu, baada ya kuwachagua viongozi wa Misingi, tawi, Kata wilaya na mkoa kwa lengo la kufanya maandalizi ya uchaguzi wa serikali za mitaa na ule wabunge na Rais.
Akizungumza na wajumbe wa mkutano mkuu wa wilaya Mwenyekiti wa Chadema wilaya ya Chato Steven Nyororo na Katibu wa chama hicho, Mange Ludomya wamesema uwepo wa viongozi wa chama hicho kuanzia ngazi za Misingi kutakiwezesha Chadema kupata ushindi wa kishindo katika chaguzi zake.
Kwamba mkakati huo iwapo utatekelezwa kikamilifu upo uwezekano wa kumwondoa Dk John Magufuli kwa madai ameliongoza jimbo hilo kwa zaidi ya miaka 15 na kwamba hana jambo jipya la kuwatumikia wananchi wake ambao wanakabiliwa na uhaba wa maji safi na salama kwa zaidi ya mika 50 iliyopita.
NIPASHE
No comments:
Post a Comment