Thursday, January 3, 2013

Mnyika awafunda vijana


MBUNGE wa Ubungo, John Mnyika (CHADEMA), amewahimiza vijana na asasi zao kuwasilisha ombi bungeni ili Bunge liweze kujadili na kupitisha mpango wa taifa wa ajira kwa vijana kwa lengo la kupunguza tatizo la ajira nchini.
Mnyika alitoa ushauri huo juzi katika ofisi ya Asasi ya Maendeleo Ubungo (UDI) katika shughuli ya kutangaza washindi na kukabidhi zawadi kutokana na shindano la vijana wasio na ajira na waishio katika mazingira magumu lililoendeshwa na asasi hiyo.
Akijibu risala iliyosomwa na Ofisa Uwezeshaji wa UDI, Goodluck Justin, aliyetaka wabunge waungane kwa pamoja kuendelea kufuatilia utekelezaji wa serikali baada ya kupokea pendekezo la kuanzisha benki ya vijana, ili kupanua wigo wa vijana kupata mikopo ya mitaji kwa ajili ya kujiajiri.
Mnyika aliielezea UDI kuwa tayari alishafuatilia suala hilo na kutoa changamoto kwa vijana kuongeza msukumo kwa upande wao ili hatua za haraka zaidi ziweze kuchukuliwa.
Mnyika alisema wakati umefika kwa vijana kuacha kulalamika na badala yake kuchukua.
Mnyika aliwaasa vijana kuwa badala ya kufikiria kuhusu benki ya vijana ni muhimu kuwa na mpango wa taifa wa ajira kwa vijana ambao ndani yake kuwe na mikakati na shughuli kadhaa ikiwamo kuanzisha hiyo benki.

No comments:

Post a Comment