Mbunge wa Nyamagana na Mkurugenzi wa mambo ya nje wa Chadema Ezekiah Wenje amesema kwamba chama chake hakina mgogoro wowote.
Akihutubia umati wa watu katika mkutano mkubwa wa hadhara wa wafuasi wa Chadema Gongolamboto DSM Wenje alisema kwamba kilichopo ni baadhi ya viongozi wa CCM kuwanunua baadhi ya watu wasio waaminifu na wenye njaa na kuanza kuropoka hovyo mambo ya kijinga kwenye vyombo vya habari.
Wenje alisema bahati njema wasaliti wote wanafahamika na taratibu za kuwashughulikia zinaendelea kufanywa dhidi yao.
Chadema wanaendelea na operesheni kubwa za M4C huku viongozi wake mashuhuri wakiwa maeneo mbalimbali ya nchi.Viongozi walioko maeneo mbalimbali wakihaha kuimarisha chama ni Godbless Lema,John Heche,James Millya na Alphonce Mawazo walioko maeneo mbalimbali ya Kanda ya ziwa.Wengine ni Tundu Lissu,Peter Msigwa na Joseph Mbilinyi wanaohaha maeneo ya nyanda za juu kusini.Pia mbunge Vicent Nyerere alikuwa akizunguka mikoa kadhaa kuimarisha chama.Naye Mkiti wa chama Freeman Mbowe alikuwa Karatu.
No comments:
Post a Comment