Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama, Halima Mdee (Mb) anaendelea vyema na matibabu katika Hospitali ya Aga Khan baada ya kufanyiwa upasuaji siku ya Ijumaa, Juni 7, mwaka huu akiwa amelazwa hospitalini hapo tangu Alhamis, wiki hii.
Mhe. Mdee ambaye ni Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake (BAWACHA) Taifa na Mbunge wa Jimbo la Kawe, alilazimika kufanyiwa upasuaji baada ya kushauriwa na madaktari wake kwa ajili ya kutibu ugonjwa uliokuwa unamsumbua.
Baada ya upasuaji huo uliochukua takriban muda wa saa 4.30, Mhe. Mdee bado yuko chini ya uangalizi wa madaktari, akiendelea kuimarika na kupata nguvu, ambapo madaktari wameshauri apate muda wa kupumzika kabla hajaruhusiwa kutoka hospitalini hapo.
Imetolewa leo Jumamosi, Juni 8, 2019 na;
Tumaini Makene
Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano
CHADEMA
No comments:
Post a Comment