Thursday, November 29, 2018

UAMUZI RUFAA YA MBOWE NA MATIKO KUTOLEWA KESHO

Baada ya jana kesi hiyo kuahirishwa leo tena imeahirishwa ambapo Mahakama Kuu Kanda ya Dar itatoa uamuzi wa rufaa hiyo kesho Novemba 30

Katika kesi hiyo, upande wa Jamhuri imeweka pingamizi la awali ukiwasilisha hoja tatu za kutaka rufaa hiyo itupiliwe mbali bila hata kusikiliza msingi wake

Katika hoja ya kwanza, Wakili wa Jamhuri, Dkt. Zainabu Mango amesema kuwa taarifa ya kusudi la kukata rufaa si sahihi

Pia, Wakili wa Jamhuri Wankyo Simon amesema rufaa hiyo haijakidhi matakwa ya kisheria kifungu cha 362(1) kuhusu mwenendo wa shauri kuambatanishwa katika rufaa

Aidha, Mawakili wa Utetezi, Peter Kibatala, Dkt. Nshalla Lugemeleza na Jeremiah Mtobesya Wamejibu hoja za mapingamizi hayo huku Jaji akisema atatoa muongozo kesho asubuhi

No comments:

Post a Comment