Chama cha Demokrasia
na Maendeleo -CHADEMA.
Taarifa kwa umma
kuhusu hafla ya uzinduzi wa Sera za Chama toleo la Mwaka 2018.
Tarehe 25.09.2018
Mwenyekiti wa Chama Taifa Mhe.Freeman Mbowe ataongoza tukio la kuzindua Sera za
Chama toleo la Mwaka 2018.
Katika kufanikisha
tukio hilo wadau mbalimbali wamealikwa zikiwemosekta na taasisi mbalimbali za
umma, sekta binafsi, taasisi na asasi za kimataifa, Balozi mbalimbali, Vyombo
vya Habari, taasisi za dini na taasisi za kitaaluma.
Aidha tumealika Vyombo
na taasisi mbalimbali za Serikali kama Mkuu wa Jeshi la Polisi, Gavana wa Benki
Kuu, Msajili wa Vyama vya siasa na taasisi nyingine kadhaa za ndani.
Katika uzinduzi huo
ambapo Chadema itaweka hadharani misimamo ya kisera kwenye maeneo mbalimbali ya
uchumi, afya, elimu na sayansi, miundombinu, maji, mfumo wa Utawala, Katiba na
haki za binadamu, Masuala ya Muungano, Mambo ya Nje na Uhamiaji, Siasa za
ndani, Usimamizi wa Ardhi na Kilimo pamoja na Mazingira.
Aidha baada ya mialiko
mbalimbali kuwasilishwa kwa wadau mbalimbali, tumestushwa na taasisi ya
Elimu (Chuo Kikuu cha IFM) kutoa tangazo na kulilipia kwenye Vyombo vya
Habari kuwa wao sio taasisi ya kisiasa na hivyo hawatashiriki kwenye uzinduzi
huo.
Kama Chadema tunaamini
kuwa taasisi zetu za elimu zina wajibu wa kusoma na kufanya tafiti mbalimbali
za kisomi kuhusu Sera za Vyama vya siasa ili waweze kuwajibu kwa ufasaha
wanafunzi wao kuhusu Sera za Vyama na utekelezaji wake, hivyo hawapaswi
kujitenga na michakato ya kisera ya Vyama vya Siasa kwani Sera huzaa dira na
mipango ya Maendeleo ya Taifa.
Tunawaalika wadau wote
wa Maendeleo ya taifa wazipitie Sera zetu na kutoa maoni, ushauri na
mapendekezo kwani tunajenga Taifa moja.
Imetolewa na;
John Mrema -
Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje.
24 Septemba, 2018
No comments:
Post a Comment