Na
Mwalimu John Pambalu.
Dunia imeshuhudia
uwezo wa ajabu wa viongozi wawili , mmoja akiwa kocha wa timu ya wa club ya
Manchester united ya nchini uingereza na mwingine akiwa kocha wa siasa za taifa
la Tanzania Sir Freeman A. Mbowe.
Ferguson meneja wa
zamani wa club ya Manchester united alipata heshima kubwa kwa kuvunja rekodi ya
kuinoa timu ya Manchester united kwa miaka takriba 27 kwa mafanikio makubwa.
Mbowe pia ndiye
mwanasiasa bora zaidi nchini Tanzania na Afrika ya mashariki kwa kukiongoza
chama kikuu cha upinzani kutoka mwaka 2004 mpaka sasa kwa mafanikio makubwa
sana. Ameitoa chadema kutoka chama kisichokuwa na uwezo wa kusimamisha mgombea
urais (chama cha kudandia wagombea wa NCCR MAGEUZI mwaka 1995 na chama
cha CUF mwaka 2000) mpaka kufikia hatua ya kusimamisha wagombea urais mwaka
2005,2010 na 2015 huku matokeo ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 yaliyotangazwa na
tume ya taifa ya uchaguzi yakidai eti Chadema ya Freeman Mbowe ilipata zaidi ya
kura 6,000,000 tu dhidi ya 8,000,000 za CCM.
Ferguson anakumbukwa
zaidi na washabiki wa soka duniani kote kwa mataji aliyobea kama mataji 13 ya
ligi ya uingereza, 2 ya klabu bingwa ulaya na 5 kombe la FA. Aidha Ferguson
anakumbukwa zaidi kwa uwezo wake wa kuibua kulea na kuendeleza vijana chipukizi
kama wakina *David Beckham, Christian Ronaldo, Van der sar, Ferdinand,
Vidic, Evra, Rooney, Giggs* na wengine wengi.
Pia Freeman Mbowe
anaheshimika zaidi kwa kuibua, kulea na kuendeleza vijana kama *John
Mnyika, John Heche, John Mrema, Benson Kigaila, Halima Mdee, Ezekia Wenje,
Zitto Kabwe, David Silinde* na wengine wengi.
Siraha kubwa
wanayoitumia miamba hii ya mifumo ya ushindi ( Ferguson na Mbowe ) ni kusimamia
nidhamu kuliko tukuka.
Mwaka 2009 Christian
Ronaldo akiwa mchezaji bora kuliko wote duniani alitaka kujiona yeye ni bora
kuliko timu. Ferguson akaamua kumuuza ili kuwafundisha wachezaji wanaobaki kuwa
hakuna supper star zaidi ya timu ya Manchester united. Maamuzia kama haya
yalifanywa mwaka 2015 dhidi ya Dr. Slaa aliyekuwa katibu mkuu mahiri sana.
Mbowe akasimamia maamuzi ya vikao kwamba hayupo aliye bora zaidi ya Chadema.
Aidha vuguvugu la
wanaaiasa wa upinzani kuhama vyama vyao masalani Chadema na kujiunga na CCM,
pia yanathibitisha uwezo wa Freeman Mbowe.
Itakumbukwa kuwa
utaratibu wa kupitisha wagombea wanaowania nafasi za uwakilishi bungeni na
katika halmashauri, wawakilishi wa vyama hupitishwa baada ya kupigiwa kura za
maoni ndani ya vyama.
Umefika wakati
wawakilishi wakijiudhuru kutoka Chadema wanateuliwa na CCM bila kupitia
mchakato wa kura za maoni.
*Hii ni ishara wazi
kuwa hata CCM wanatambua kuwa vijana waliopita mikononi mwa Mbowe wanauwezo
mkubwa kuliko vijana na wazee walioko CCM.*
Ndio maana
wanaotokea Chadema wanapata teuzi za ukuu wa wilaya, ukatibu tawala nk.
Huku waliokulia CCM wakiendelea kuzeeka bila teuzi.
Ferguson na Mbowe
wanabaki kuwa alama ya uwezo wa taasisi walizoziongoza (Manchester United na
Chadema)
Tangu alipong'atuka
madarakani Ferguson mpaka leo club ya Manchester united imepoteza mwelekeo
wake, kosa ambalo taasisi ya Chadema haiko tayari kulifanya hata kidogo.
Wasalaam
John Pambalu.
Diwani wa kata ya
Butimba Mwanza
Makamu Mkt Bavicha
Tanzania bara.
Mshabiki wa Manchester
United
No comments:
Post a Comment