Wednesday, March 14, 2018

Baraza la Wazee CHADEMA lamtaka Rais Magufuli aongoze kwa busara na hekima ya mtu mzima, ladai kauli zitawapeleka ICC

Baraza la wazee wa CHADEMA kupitia kwa katibu mkuu wake, Lodrick Rutembeka wamezungumzia kukamatwa, kubambikiziwa kesi, kuteswa, kutekwa, kushambuliwa hata kuuawa kwa viongozi wa kisiasi hata wananchi wengine wanaoonekana kukosoa utendaji wa kazi wa Rais Magufuli na serikali kwa kutumia rejea ya matukio kama la Tundu Lissu, kuuawa kwa kaimu mwenyekiti wa CUF jimbo la Matopetope, Ali Juma Suleyman.


Pia miili ya watu waliouawa iliyokuwa ikiokotwa kwenye fukwe ilhali serikali ikitoa taarifa tatanishi na taarifa zinazotoa majibu mepesi kwa maswali magumu. Ikiwemo kusema wanaookotwa ni wakimbizi.

Tatu ni kuminywa kwa haki za kikatiba na kisiasa kinyume na sheria za nchi, mfano kuzuiliwa kwa shughuli za kisiasa. Nne ni kuminywa kwa uhuru wa maoni na kupata taarifa ikiwemo kuzuiwa Bunge mubashara na kufungwa kwa magazeti.

Mihimili ya mahakama na bunge kuingiliwa na mhimili wa serikali.

Baraza la wazee CHADEMA limesema halitonyamaza kimya kwani yamkini serikali inaweza ikasikia, limetoa ushauri kwa Rais na serikali kuchukua hatua kwani ni vizuri kusikiliza kelele na kilio kwenye mitandao pamoja na mikutano ya hadhara kupigwa marufuku kwani na kutoa kauli tata zinaweza kuwapeleka mahakama ya ICC. BARAZA LIMESHAURI


1. Rais Magufuli ambae ni mzee mwenzao aongoze kwa busara na kiongozi na hekima ya mtu mzima. Akubali kuitikia wito wa kukutana na wazee katika kikao kimoja ambao watakuwa na ujasiri wa kumwambia ukweli na kutoa ushauri wa kulipusha taifa kuelekea katika janga. Wamesema kukubali kuzungumza sio kukubali kushindwa na kutolea mvutano kati ya Marekani na Korea kaskazini pia nchini Kenya ambapo Rais wa Kenya amekutana na mpinzani mkuu kuzungumzia tofauti zao.


2. Awe tayari kusikiliza na kupokea ushauri na ukosoaji kama alivyo tayari kupokea hongera pamoja na kupata sifa ya kuweza kuongoza malaika mbinguni.


3. Kwa ajili ya kutibu majeraha na kuondoa makovu yanayosababishwa na mwenendo wa kisiasa nchini kwa sasa, suluhu la kudumu ambalo litaweka taifa pamoja ni katiba hivyo ni wakati muafaka kuzungumzia katiba mpya kuelekea uchaguzi wa 2020.No comments:

Post a Comment