Friday, February 23, 2018

PUMZIKA KWA AMANI GODFREY LWENA
Marehemu Godfrey Luena Diwani wa CHADEMA Namawala, alifunguliwa kesi nyingi na zote alikuwa anashinda. Ni Diwani aliyekuwa na ushawishi sana na wananchi. Juhudi za kumnunua zilishindikana. Kutoka Ifakara mjini mpaka Namawala ni KM 20+ lakini polisi imewachukua masaa 3 na nusu kufika. Mauwaji ya Godfrey yana ukakasi sana angekubali kununuliwa kesi zake zingefutwa labda angekuwa hai. Godfrey amekufa akitetea itikadi yake. Godfrey aliweza shawishi wananchi wagomee michango isiyo na maana na alikuwa mtetezi wa wapiga kura wake. 

No comments:

Post a Comment