Wednesday, December 6, 2017

Mbunge wa Ubungo, Saed Kebenea(CHADEMA) akanusha kujivua uanachama wa CHADEMAMbunge wa Ubungo, Saed Kebenea(CHADEMA) amekanusha tetesi kuwa yuko kwenye mpango wa kuhamia CCM. Amesema kinachoenezwa sasahivi ni propaganda ili kukitoa chama chake kwenye ajenda ya kuhoji mambo ya msingi.

“Sijawahi kumweleza mtu kwamba nina mpango wa kuhama CHADEMA, wala sifikirii, sijawahi kukaa na CCM na hayo mambo nayaona kwenye mitandao, kama kuna mtu ana ushahidi wa mimi kuzungumza na CCM autoe, sina sababu za kuhama, imani niliyopewa na Ubungo ni kubwa, siwezi kuichezea,”

"Kama nikutaka kuondoka CHADEMA nitaondoka kwa hiyari yangu na sio kwa kununuliwa na CCM. Nimejenga jina langu kwa miaka zaidi ya 15. Siwezi kuwasaliti wananchi wa Ubungo"

"Kuna watu kama Lowasa,Sumaye nimeshiriki kuwatoa CCM na kuwaingiza CHADEMA.Leo nikienda CCM watanielewaje"?

"Absalom Kibanda Ndiye mwanzilishi wa hizi propaganda za mimi kuhamia CCM.Nilimuonya asinichafue kwani namheshimu"

"Mbunge Godbless Lema ndiye amekuwa kinara kuzungumza haya mambo kwenye mitandao ya mimi kuhama hivyo kuleta taharuki kwenye mijadala ya wabunge wa CHADEMA". Amesema Kubenea.

No comments:

Post a Comment