Wednesday, November 8, 2017

Mbunge cecil D. Mwambe Ashikiliwa na Polisi Mtwara


Mpaka sasa Mhe. Cecil D. Mwambe (Mb) bado anashikiliwa na Jeshi la Polisi na amewekwa mahabusu kituo cha Kati hapa Mtwara.

Awali aliitwa na RCO Mtwara kwa mahojiano kwa sababu ya hotuba yake ya jana 07.11.2017 katikamkutano wa ufunguzi wa kampeni za Udiwani Kata ya Reli hapa Mtwara Mikindani.

RPC hakuridhika na mahojiano ya takribani saa tatu na nusu (6:00 hadi 9:300) yaliyofanywa na wasaidizi wa RCO. Hivyo RPC akaagiza awekwe rumande na RCO amhoji upya.

Mahojiano yalifanyika mbele ya Wakili Songea

Mpaka sasa bado yuko rumande na mahojiano mapya hayajafanyika.

Philbert Ngatunga
Katibu wa Kanda, Kusini
CHADEMA

No comments:

Post a Comment