Wednesday, November 15, 2017

Lowassa: CCM waliiba kura na sasa ninaomba serikali ya umoja wa vyama.



Aliyekuwa mgombea Urais wa Tanzania kwa tiketi ya CHADEMA, Edward Lowassa amependekeza kuwepo na katiba Mpya inayowezesha uundwaji wa serikali inayojumuisha vyama vyote vya siasa tofauti na sasa ambapo mshindi ndiye pekee anayeunda serikali.

Edward Lowassa ameyasema hayo wakati akihutubia katika mkutano wa hadhara wa kumnadi mgombea udiwani wa tiketi ya CHADEMA katika kata ya Moita katika Halmashauri ya Monduli yenye wapiga kura 4,417.

Lowassa amerudia kauli yake na kudai kuwa CCM waliiba kura zake lakini hata kura walizompatia ambazo ni zaidi ya milioni sita zinamfanya awe sauti ya wananchi hao ambapo kama katiba ingekuwa inazingatia matakwa ya sauti ya wananchi wote alitakiwa awe mmoja wa watu wanaounda serikali ya umoja nchini.

Amewaasa wanachama na wapenzi wa CHADEMA wazilinde kura katika uchaguzi huu mdogo wa madiwani kwa sababu bila kuzilinda zitaibiwa kama alivyoibiwa kura zake katika Uchaguzi Mkuu 2015.

Kilichoshangaza kidogo kwa sasa ameachana na moto yake inayosema ''Lowassa Mabadiliko, Mabadiliko Lowassa huku wafuasi wake wakizungusha mikono. Ambacho hakijabadilika ni kushikiwa microphone wakati akihutubia!

No comments:

Post a Comment