Wednesday, November 22, 2017

Edward Lowassa: Wanaodhani nitarudi CCM Wanapiga porojo na kuota ndoto

Waziri Mkuu mstaafu na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA, Mh. Edward Lowassa leo amefika katika kata ya Makiba akiambatana na Mbunge wa Arumeru Mh. Joshua Nassari, Mbunge wa Simanjiro Mh. James Milya na baadhi ya viongozi wa chama wa kanda ya Kaskazini ili kumnadi mgombea udiwani wa kata hiyo Bi. Joyce Rutha.

Hii ni sehemu ya aliyoongea:

Edward Lowassa: Leo Nimeona kwenye mitandao ya kijami kuna mtu anasema nimemtumia watu wamueleze kwamba nataka kurudi CCM, siwezi kurudi CCM hayo ni maneno ya Kipuuzi na Ndoto za mchana

Edward Lowassa: Nikajiuliza hata Patrobass Katambi? Nikagundua ooohh Kumbe ni Msukuma... Ndio Maana

Edward Lowassa: Ninaiomba Serikali ya CCM iache mara moja kutuongoza kwa ukabila taifa letu halikujengwa katika misingi hiyo

Edward Lowassa: Hatuwezi kugombana na kuchukiana kwasababu ya Kuhama vyama na wala tusikubali kubaguliwa hivyo, sisi ni Watanzania Kwanza. Lakini binafsi bado naamini Mabadiliko ya kweli yatatoka nje ya CCM.

No comments:

Post a Comment