Friday, September 15, 2017

TAARIFA KUHUSU HALI YA TUNDU LISSU KWA SASA

Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amesema kuwa hivi sasa Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu anaweza kuongea na kula kidogo.

Akizungumza na waandishi leo Alhamisi jijini Nairobi, Mbowe amesema taarifa za kwamba Lissu amepata maambukizi katika kifua ambayo yanatishia maisha yake siyo za ukweli.
Mbowe amesema hali ya Lissu inabadilika kila siku hivyo amewahakikishia wananchi kuwa anaendelea kurejea katika hali yake.
Amesema Lissu ameweza kuonana na baadhi ya waliomtembelea kwa maelekezo ya madaktari ambao wanamtibu.

"Pamoja na kwamba kuna watu wengi wanataka kumuona lakini ni wachache wanaoruhusiwa kumuona kwa kuwa madaktari wanataka apumzike,"amesema Mbowe.

No comments:

Post a Comment