Wednesday, September 27, 2017

Godbless Lema amkataa hakimu adai ana maamuzi ya hila yaliyomfanya asote rumande miezi 4

HAKIMU Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Arumeru, Desderi Kamugisha amegoma kujitoa kusikiliza kesi ya uchochezi inayomkabili
Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema(CHADEMA) licha ya mbunge huyo kumtaka afanye hivyo kwa kile alichodai kuwa aliwahi kufanya maamuzi kwani hila yakampelekea kusota maabusu zaidi ya miezi minne.

Aidha hakimu huyo aliamua kuendekea na shauri hilo hata pale mawakili wa Lema walipowasilisha kwa mdomo kusudio la kukata rufaa Mahakama Kuu kwa lengo la kupinga uamuzi huo mdogo.

Hayo yalijitokeza jana wakati shauri hilo lilipokuja mahakamani hapo kwa ajili ya Lema kusomewa hoja za awali huku upande wa Jamhuri ukiwakilishwa na wakili, Khalili Nuda na Alice Mtenga.

Wakili wa Lema, John Mallya aliieleza mahakama kuwa hoja ya mteja wake kuwa hakimu Kamugisha alitoa maamuzi ya hila dhidi yake yanapewa uzito na maamuzi ya mahakama Kuu yaliyotolewa na Jaji Salma Magimbi aliyeweka wazi kuwa mahakama ilishindwa kutumia vizuri mamlaka yake hivyo kukubali kuingiliwa na Kumkataa hakimu Kamugisha kwani

Katika hoja ya pili wakili wa Lema aliieleza mahakama kuwa kuna shauri lingine hakimu huyo aliwahi kumpa haki ya dhamana mteja wake ambapo waliomba ahirisho fupi ili aweze kutekeleza masharti hayo kwa kutafuta wadhamini lakini hakimu huyo hakusema kama amekubali au amekataa ombi hilo badala yake alienda kusaini hati ya kumpeleka rumande.

Hata hivyo alifanikiwa kukidhi masharti ya kabla utekelezaji wa yeye kupelekwa mahabusu haujafanikiwa ingawa alitumia nguvu.

"Ilibidi mteja wetu atumie nguvu kuingia kwenye mahakama yako ili akamilishe masharti yake ya dhamana huku akinyooshewa mtutu wa bunduki na OC CID wa wilaya ya Arusha,Damas Massawe,mteja wetu anatoa rai kwamba haoni kusikiliza kesi hii iliyopo mbele yako kama utaisikiliza kwa haki na usawa," alisema wakili Mallya.

Alisema hakimu huyo ndiyo akifanya maamuzi kwenye kesi mbili za mteja wake ambazo maamuzi yake yamekuwa ya kihistoria hivyo kusisitiza ,"natoa rai kwa heshima mahakama yako wewe ujitoe kusikiliza kesi hii ili Hakimu mwingine apangiwe kesi hii ili aweze kusikiliza bila kuwa na hila,".

Wakili wa Serikali Nuda aliitaka mahakama itupie mbali hoja hizo kwani anaamini hakimu alitoa uamuzi kwa kuzingatia sheria huku akidai kuwa mawakili wa Lema wana nia ya kuchelewesha usikilizwaji wa kesi.


Hakimu Kamugisha akitolea uamuzi mdogo hoja hizo alisema kuwa hazina mashiko hivyo kuzitupankwa kile alichoeleza kuwa jaji au hakimu hawezi kujitoa kwa sababu za kudhania kufikirika au zinazotokana na uoga.


"Mahakimu na majaji japo ni wasomi wa sheria huwa wanafanya makosa ya kisheria ndiyo maana tunasema mtu asiporidhika na uamuzi wa mahakama anakata rufaa ambapo anaweza kuwa na sababu za aina mbili za mantiki au kisheria," alisema hakimu huyo na kuongeza.


"Mshitakiwa anapopewa dhamana anatakiwa akatimiza dhamana na hilo ndilo lililofanyika baada ya kutimiza masharti ya dhamna na lakini baada ya kutimiza masharti alioewa,kwa sababu hizo mbili sioni msingi wa hila,kwa maana hiyo maombi ya mshitakiwa ya kujitoa kwenye kesi hii nimeyakataa na kesi itaendelea mbele yangu,".

Baada ya uamuzi huo wakili Mallya anayemtetea Lema aliieleza mahakama hawajaridhika na uamuzi huo hivyo akawasilisha kusudio la mdomo la kukata rufaa mahakama Kuu.

Hakimu Kamugisha alisema hawezi kuzungumzia uhalali wa maombi hayo hivyo akaagiza shauri hilo kuendelea mahakamani hapo huku wakisubiri mawakili wa Lema wamalize mchakato wa rufaa.

MASHAHIDI TISA NA VIELELEZO VITATU KUWASILISHWA

Wakili wa Serikali, NudhuuBakarimea Lema hoja za awali alisema kuwa wanatarajia kuleta mahakamani hapo mashahidi tisa na vielelezo vitatu kuthibitisha mashitaka hayo.


Aliwataja mashahidi hao kuwa ni Mkuu wa Upelelezi wa Wilaya ya Arusha(OC CID),Damas Massawe, Joseph Labia, W 7006 DC Tausi Hussein na H 2263 PC Musa ambao wote ni askari wa Kituo cha Polisi cha Kati jijini hapa.

Wengine ni Inspekta Aristedes Kasigwa kutoka Francis Bureae, Makao Makuu ya Polisi jijini Dar Es Salaam, Silvester Meda mkazi wa Sanawari, Lilian Joel (Kaloleni), Bakari Juma(Kwa Mrefu),Gofrey Laizer(Baraa).

Wakili Nuda alitaja vielelezo watakavyotumia kwenye shauri hilo kuwa ni pamoja na digital video casset ,(DVC), aina ya Sony, kamera aina ya Sony DVCAM yenye serial namba 7.2 V 222470 na ripoti ya uchunguzi ya kitaalamu ya tape ya video.

Shauri hilo limeahirishwa mpaka Oktoba 9, mwaka huu ambapo mashahidi hao wataanza kutoa ushahidi wao.

Lema anadaiwa Oktoba 23 Mwaka jana katika mkutano wa hadhara viwanja vya Shule ya Sekondari Baraa, Lema alitoa maneno kuwa; “Kiburi cha Rais kisipojirekebisha, Rais akiendelea kujiona yeye ni Mungu, Mwaka 2020 haitafika Mungu atakuwa ameshamchukua maisha yake.”

“Rais ana kiburi, Rais kila mahali watu wanaonewa,wafanyakazi wa serikali hawana amani, wafanyabiashara hawana amani,watu wananyanyaswa.”Lema alinukuliwa na Wakili wa Serikali, Mtenga.

No comments:

Post a Comment