Wednesday, September 13, 2017

CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA) TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI, JUU YA TUKIO LA KUVAMIWA KWA MEJA JENERALI MSTAAFU VICENT MRITABA.


CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA) TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI, JUU YA TUKIO LA KUVAMIWA KWA MEJA JENERALI MSTAAFU VICENT MRITABA.

Tumepokea Taarifa za kuvamiwa kwa Meja Jenerali Mstaafu Vicent Mritaba na kupigwa risasi, kwa mshituko mkubwa na hasa kutokana na ukweli kuwa tukio hili limetokea Katika kipindi hiki ambacho sisi CHADEMA na watanzania wote tukiwa kwenye Taharuki na huzuni kubwa iliyosababishwa na jaribio la kutaka kumuua Mhe. 

Tundu Lissu Akiwa Dodoma wiki iliyopita. Tunalaani kwa nguvu zote uhalifu huo na tunaungana na Familia ya Meja Jenerali Mritaba na watanzania wote kumuombea aweze kupona na kurejea Katika majukumu yake ya kujenga taifa. 

Aidha tunavitaka vyombo vya dola kuchunguza na Kuwatia hatiani wale wote waliohusika na uvamizi huo ili kuhakikisha kuwa usalama wa raia na Mali zao hauko shakani. Imetolewa Leo Jumanne, tarehe 12 Septemba,2017 John Mrema 

Mkurugenzi wa Uenezi, Mawasiliano na Mambo ya Nje .

No comments:

Post a Comment