Wednesday, August 2, 2017

Geita: CHADEMA wavuna wanachama 60 wa CCM, wengi wajihusisha na Tundu Lissu

Leo katika sherehe ya vikundi Katika Tawi la Nyantorontoro B jimbo la Geita mjini tumepokea wanachama Wa ccm 60 na kuwakabidhi za Chadema.

Wamesema wameamua kuungana na wana mabadiliko hasa Tundu Lisu kupigania Demokrasia na wao hawapendi udikteta.

Wamesema serikali ya ccm imekuwa inawaonea sana wapinzani wamekuwa wanawatisha sana wapinzani wameamua kuungana na upinzani ili wawatoe ccm.

Maana wameona wapinzani hawana matatizo kwani wameongozwa na Mwenyekiti serikali ya mtaa tangu 2014 wa Chadema hawabagui ila ccm wanawabagua wapinzani .

Wamesema walidanganywa na ccm wataletewa kila kijiji 50 lakini kumbe ulikuwa ni uongo tu hali ya maisha imekuwa ngumu sana.

Kadi hizo wamekabidhiwa na Mwenyekiti Wa Wilaya Ndg Amos Nyanda akishuhudiwa na Mwenyekiti Wa Bavicha Wilaya ya Geita Kamanda Mhere Mwita.

Katika sherehe hiyo vikundi vya Ujasiriamali ambayo vina wanachama wapatao 100 Chadema tumeweza kuwapatia Fedha pamoja na Sehemu ya kufugia kuku wa mayai kama sehemu ya Mradi.

Vile vile Uongozi wa chadema Wilaya ya Geita uliwakabidhi wakina mama wajiriamali vyeti vya kutambua Mchango wao katika kuleta maendeleo katika mataa vilivyotengenezwa na Chadema jimbo la Geita mjini.

Imetolewa na:~
Mimi Mhere Mwita
M/Kiti Bavicha (W) Geita
02/08/2017

No comments:

Post a Comment