Saturday, July 15, 2017

Ni nini kipya CCM imefanya tangia 2015 ? Ndo yale Mw. Nyerere alisema, msiposimama na kuwa wamoja na kutakaa upuuzi, tutatawaliwa na Madikteta. Sisi tunakubaliana na kauli ya Mw Nyerere na tunasema Chadema na UKAWA 2020 !

Wapendwa Niwasalimu wote kwa jina la Bwana;

Na kwa wana Chadema na Ukawa- People’s Power !
Nina maoni machache tu kutokana na yanayondelea sasa:

Tuko pamoja kama watanzania kuhakikisha haki inapatikana kwa viongozi wetu wote wa Chadema na Ukawa. Isiwapeni tabu kwa maana Bwana Yupo pamoja nasi.

Mungu hapimi kwa mambo ya nje, au yale yanayofanyika nje, anapima mioyo yetu. Na yote anayashuhudia ya kwamba Chadema inafanya mema na tutatunikiwa zawadi yetu.

Sihitaji kutoa mifano mingi maana najua tayari mifano mingi mnaijua; viongozi wengi duniani hata kwenye Biblia walikamatwa na watu waovu kwa kusimamia ukweli tu nay ale wanayoamini. Na tukaona mwisho wa siku Baraka na mavuno makubwa ya ushindi waliopata. Hivo kazeni buti, ushindi ni wa kwetu 2020.

Kuhusu hao madiwani wa Chadema wanafiki, waacheni maana CCM hawawezi kuwanunua wananchi wapiga kura. Wananchi watakula pesa zao nab ado kupigia Chadema. Kwanza imekuwa vizuri wamejiondoa mapema ili tujua mapema nani ni msaliti na asiuze siri cha chama.

Kama mnakumbuka Nigeria, kwenye uchaguzi wa 2015, Chama kilichokuwa madarakani kilihonga mabilioni ya pesa kwa wanasiasa na vyama vya upinzani. Zote zikaliwa na alishinda alikuwa ni Buhari wa Upinzani.

Kwa hiyo kuhonga kwa sisi wakisto haijalishi, tena hasa ni mbaya maana ni machukizo kwa Mungu. Hivo CCM wanazidi kujipalia makaa ya moto kama kweli wanawanunua hawa Madiwani wa Chadema kwa pesa zetu sisi watanzania.

Ni Dhahiri kwamba hao madiwani wa Chadema waliokuwa wasaliti hawajitambui na hawatumii akili na nitawaambia kwa namna zipi:

· Watawezaje kuunga mkono Raisi kwa kuacha kazi waliotumwa na Wananchi.

· Watawezaje kuunga mkono chama ambacho kimewadhalilisha na kuwaonea miaka yote hii.

· Watawezaze kuunga mkono Raisi anayevunja sheria za nchi na kutofata katiba.

· Wanawezaje kuunga mkono uovu wote unaofanywa na CCM, na wanaona kila siku Chadema ndio wanaoibua uozo wa CCM bungeni.

· Wanawezaje kuunga mkono chama cha CCM kinacho abuse power kama Bashite na Raisi hafanyi kitu.
Wanawezaje kuunga mkono CCM ambayo imewadhalilisha CUF Zanzibar, kutumia nguvu kupiga na hata kuuwa watu kukaa tu madarakani.

· Wanawezaje kuunga mkono chama ambacho kinashuhudia utekaji wa wana Chadema wenzao wakina Ben Sanane mpaka leo hatujui walipo, leo wanaunga mkono hicho chama.

· Wanawezaje kuunga mkono CCM inayokamata viongozi wa chadema kama Lowassa, Halima, na Wakina Lissu, na kuwaharibia mashamba wakina Mbowe.

Kibiti imewashinda, kuna mauaji kila siku, wako busy na wapinzani. Ndo sasa unapata kuona namna gani uongozi uliopo madarakani Tanzania haupo serious na kuwalinda wananchi, bali kuwalinda mafisadi wakina Tibaijuka na Chenge. Halafu wanaleta geresha za kurudisha milion 50 wakati mapapa wakubwa wanawalinda.

Na bado mtu mzima mwenye akili zake timamu anaunga mkono haya?

Ni nini kipya mabacho Magufuli kafanya tangia kaingia madarakani? Zaidi tu ya kuzidi kuvunja sheria na kuzidi watu kuonewa, kutekwa na kunyamazishwa?

Hata yale ambayo wanafikiri Magufuli kafanya au anafanya, mtu yeyote mwenye akili akiangalia ataona ni yale yale ambayo Chadema imekuwa ikiyapigia kelele kwa miaka yote. Ni aliye na uwelewa mdogo sana ataunga mkono CCM kwa sasa, maana hata CCM pia wameamka na ndani yao wanaona tofauti zao.

Hata hiyo ya watoto wanaopata mimba, in fact iko kinyume hata na ilani ya CCM. Sasa sieliwi hao wanaounga mkono CCM wanaunga mkono kitu gani ?

Lakini hii ndio inatufanya tuelewe ya kwamba ile ripoti ya TWAWEZA ilisema ukweli, ya kwamba watu wanaounga mkono CCM hawajielewi. Maana haiwezekani CCM inafanya uovu wote huo juu niioeleza na mwengine mwingi amabo Lissu aliuongea kuhusu rushwa, nab ado watu wanaunga mkono.

Chadema na Ukawa peke yao ndo wameibua kila uozo wa CCM, kila siku inasikia scandal za CCM kupitia Chadema na UKAWA halafu leo hii tunashangaa eti CCM wanapambwa na maua. Yaani kweli ni rushwa tupu maana mtu mwenye akili anaweza kabisa ona wazi CCM wamekwisha.

Basi niishie hapo:
Endeleeni na mapambano, kijiji hadi kijiji, endeleeni kuvuna wanachama, mkiendelea kusimamia haki na kweli. Na Bwana Yupo nasi kuhakikisha CHADEMA na UKAWA inaingia madarakani 2020. Hao CCM Waendelee kuhonga tu, wananchi watakula hela na mwisho wa siku watachagua Chadema manake watu wanaakili siku hizi na Mungu ndiye mwamuzi wa mwisho wala sio NEC.

Msikubali Hongo ya namna yoyote ile kama alisevosema mwenyekiti Mbowe. Msikubali hongo, mtende haki, na kusimama katika kweli maana hayo ndo mapendezo ya Bwana yanayowapeleka madarakani 2020. God has the final say!

Endeleeni kwa kasi kujiimarisha kila kona, mikoa, vijiji na kuwapa elimu wanawake. 

God sees your good work; your reward is coming in 2020.
People Power 2020!

May God Bless you, May God Bless the United Republic of Tanzania.

Justin Phillip

No comments:

Post a Comment