Saturday, June 10, 2017

MANISPAA YA UBUNGO YATOA KAZI ZA BILLION 4 KWA WAKANDARASI



MANISPAA YA UBUNGO YATOA KAZI ZA BILLION 4 KWA WAKANDARASI
Leo tarehe 9 mwezi wa Sita, Mstahiki meya wa halmshauri ya manispaa ya Ubungo Mh. BONIFACE JACOB

Amengia mikataba ya kazi mbali mbali na makampuni ya ujenzi, barabara na wazabuni 29.

Makampuni hayo yalisainiana mikataba mbele ya waandishi wa habari na watu mbalimbali waliofika kushuhudia tukio hilo la aina yake ambapo jumla ya mikataba 29, ilisainiwa na wakurugenzi wa makampuni mbalimbali,ambapo kati ya hayo makampuni 14 yamepewa kazi za billioni 3.2 kwa kazi ya kusafisha barabara na mazingira yote ya halmashauri ya manispaa ya ubungo ili kuifanya halmashauri ya ubungo iwe safi na yenye kuvutia.

Fedha za kiasi cha shillingi Millioni 400 ni kwa ajili uchongaji wa barabara za mitaa mbalimbali ya halmashauri ikiwemo ile maarufu ya Watani makaburini(MAKURUMLA) na Millioni 200 Ni kwa ajili ya Miradi ya upelekaji wa maji katika kata za Mbezi na Mabibo.

Kiasi kingine cha shillingi Millioni 200 no kwa ajili ya Ukarabati mfumo wa maji Hospitali ya Sinza na ujenzi madarasa ya shule ya sekondari ya Matosa (GOBA)na nyumba za walimu 6 hukohuko Matosa (GOBA).

Aidha mkurugenzi wa halamshauri aliwataka wakandarasi na wazabuni kufanya kazi zao kama masharti ya mikataba inavyotakana kwa uamanifu mkubwa.

Kusaini mikataba hadharani na mbele ya wananchi ni utekelezaji wa uwajibikaji na uwazi katika halmashauri ya manispaa ya ubungo.

Imetolewa na
OFISI YA MSTAHIKI MEYA.
HALMASHAURI YA MANISPAA YA UBUNGO.
KIBAMBA HQ

No comments:

Post a Comment