Friday, April 14, 2017

TUME YA MAADILI YAKUBALI MASHITAKA DHIDI YA RC MAKONDATUME YA MAADILI YAKUBALI MASHITAKA DHIDI YA RC MAKONDA

Ndugu waandishi wa habari, kwa heshima kubwa ya kutambua nafasi yenu muhimu kwenye jamii, nimewaita hapa ili tushirikiane kuujuza umma kwamba tupo kwenye wakati mzuri wa haki kuonekana ikitendeka dhidi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam ambae kwa vielelzo vyote anatambulika kama Daudi Albert Bashite lakini wengi wanamfahamu kama Paul Makonda.

Ndugu waandishi wa habari, huu ni mwanzo, na kwa hakika ni mwanzo mwema wenye kuashiria kuwa mwisho wa Daudi Bashite umewadia.

Ndugu waandishi wa habari, ntakumbuka kuwa 22 Machi 2017 mwaka huu, niliwasilisha mashitaka yangu dhidi ya Daudi Bashite kwa Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma, kutaka achukuliwe hatua za kinidhamu kwa kukiuka maadili ya utumishi wa umma na kukosa sifa yakuwa kiongozi si tu DSM bali Tanzania kwa ujumla.

Mashtaka yangu tume yalikuwa ni yafuatayo;

1. Kugushi vyeti vya kitaaluma kulikofanywa na RC makonda huku akijua fika kuwa vyeti anavyotumia vya taaluma si vyake wala si muhusika hivyo kujiita PAUL CHRISTIAN MAKONDA huku akijua fika kuwa yeye ni DAUDI ALBERT BASHITE, amekiuka sheria za nji nakutenda jinai.

2. Kula kiapo cha utii na uaminifu mbele ya Mheshimiwa Rais kwa uhusika wa kugushi ni kosa kubwa sana kisheria,huku akijua fika kuwa Rais alipaswa amuapishe yeye kama DAUDI ALBERT BASHITE na siyo PAUL CHRISTIAN MAKONDA.

3. Kujipatia mali kama magari na vinginevyo kinyume na maadili ya viongozi wa umma, ambapo zawadi zote unazopokea unapaswa kutangaza hadharani, ikiwemo kupata mali hizo kwa wahusika ambao amekuwa akiwatangaza hadharani na kuwatuhumu kujihusisha na uuzaji wa madawa ya kulevya.

4. Kukiuka Misingi ya utawala bora haki za binadamu na utawala wa sheria kwa kutuhumu watu ovyo hadharani kuwa walijihusisha na biashara ya madawa ya kulevya kabla ya kukutwa na hatia na kisha wengine kuachiwa huru baada ya kubainika hawakutenda makosa hayo; kinyume kabisa na sheria ambapo mtu anatakiwa kutangazwa hadharani anapokutwa ametenda makosa.

5. Shitaka la mwisho lilikuwa ni la Uvamizi wa kituo cha kirusha matangazo ya redio na runinga cha Clouds media, ambapo akijua kuwa maadili ya viongozi wa umma, hayaruhusu kiongozi kushurutisha au kulazimisha jambo lolote kwakutumia madaraka yake kama kiongozi, ambapo mtuhumiwa alitenda kosa la kutaka kutumia nguvu kurusha kipindi cha kumkashifu Kiongozi wa dini wa Maknisa ya Ufufuo na Uzima almaarufu kamam Askofu Josephat Gwajima.

Ndugu waandishi wa habari, jana Aprili 12, nilipokea barua kutoka kwa Kamishna wa Tume, *Jaji Harold R Nsekela* akinijulisha kuwa Tume ya maadili ya viongozi wa Umma imekubali Mashtaka yangu dhidi ya mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, na kunitaarifu kuwa wameanza kuyafanyia kazi mashitaka yote.

Ndugu waandishi wa habari, taarifa hiyo ya Kamishna wa Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma, imetoa mwanga mkubwa kwamba HAKI ambayo wengi wamekuwa wakiiomba, sasa Mwanga umeanza kuonekana.

Hivyo niwaombe wapenda haki wote popote walipo tushirikiane kwa hili ambalo mkuu wa mkoa amekuwa ni kero jijini Dar es salaam, Tupeane ushirikiano wa kuniongezea vielelezo vingine zaidi ya vile nilivyowasilisha Tume yaani vyeti na nakala zingine za mali kama nimesahau jambo lolote.

Mimi mlalamikaji na mashahidi wangu muhimu tupo tayari, mbali na matukio ya utekwaji na upoteaji wa watu lakini tumeendelea kutaka kuona mwisho wa kero hii jijini Dar es salaam, hivyo wakati wowote shauri litakapo anza kusikilizwa kwenye baraza la maadili ya viongozi wa umma, tutakuwa mstari wa mbele kutaka haki itendeke.

Wenu
Katika upiganiaji haki

BONIFACE JACOB
MSTAHIKI MEYA
MANISPAA YA UBUNGO

No comments:

Post a Comment