Tuesday, April 4, 2017

MEYA DAR AONYA KUWANYANYASA WAJANE

NA CHRISTINA MWAGALA, (OMJ) Dar
MEYA wa jiji la Dar es Saalaam Isaya Mwita ameonya tabia kwa baadhi ya watu kuwa nyanyasa wajane na kusisitiza kuwa wasitengwe badala yake familia zichukue jukumu la kuwasaidia kikamilifu.

Meya wa jiji ametoa kauli hiyo jijini hapa mwishoni mwa wiki wakati wa misa ya kumuaga mchungaji Leornad Lukala wa kanisa la KKKT usharika wa Ukonga , mtaa wa Mongolandege mwishoni mwa wiki.

Alisema kwamba katika familia nyingi kumekuwa na dhana potofu ya kuwanyanyasa wajane huku ndugu wa familia wakidiriki kuwadhurumu mali jambo ambalo hufanya watu hao kuishi kwenye mazingira magumu.

Aliongeza kwamba jambo hilo katika jami ya kitanzania halikubaliki na wala kuvumilika na hivyo kila mmoja anapaswa kuchukua tahadhari juu ya watu hao.

“ Kumekuwa na tabia ya watu kunyanyasa wajane , hawa watu wakishaondokewa na wenziwao , basi familia utakuta ndio zina sauti badala ya mfiwa, wanazurumu mali, ndio mana kumekuwa na kesi kadha wa kadha kwenye Mahaka zinazo shugulikia mambo ya mirasi” alisema Meya Isaya.

“ Naomba niwaombe sana, wajane wasitengwe, wapewe huduma zao kama ilivyokuwa awali, msifanye watu hawa wakajutia kubaki duniani, msitumie nafasi zenu kuwa zalilisha, wapeni huduma kama wengine” aliongeza.

Lakini sitaki kuingia mambo ya Mahakama, ila ninachotaka kueleza hapa ni kwamba , hawa watu wasitengwe, wapewe haki zao, na familia zisiwatelekeze, zichukue nafasi ya kuzihudumia, hii itakua ni kinga ya kupunguza kesi za mirasi” alifafanua.

Alisema kuendelea kuwazurumu na kuwatenga wajane, ndio chanzo cha kwenda Mahakamani kushtaki , mabaya zaidi jambo hili halitesi familia ambayo imeshtakiwa ila yule ambaye ameshtaki.

Katika hatua nyingine Meya Isaya alisema kwamba , viongozi waliopewa nafasi za kuhuumia wananchi wanapaswa kuacha alama pindi wanapomaliza muda wao.

“ Naomba sana viongoziambao tumepata nafasi za kuwatumikia wananchi, iwe ni kwenye sekta ya dini, kisiasa, serikalini, na sehemu nyingine, tujitahii sana kuacha alama kwenye maeneo yetu, ambazo zitafanya leo hii mtu akifa zinaonekana na kukumbukwa” alisema Meya Isaya.

Mchungaji Lukala alifariki dunia Machi 30 mwaka huu njiai akipelekwa kwenye kitiuo cha afya cha Mongolandege ambapo atazikwa leo kijijini kwao Mwanalumango Kisarawe mkoani Pwani.

Awali Meya Isaya alitembelea ofisi ya Kata ya Ukonga na kufanya mazungumzo mbalimbali na Diwani wa kata hiyo Juma Mwipopo,ambapo mazungumzo hayo yalilenga kuziwezesha kata ili kutatua changamoto mbalimbali zinazo wakabili.


No comments:

Post a Comment