Tuesday, March 14, 2017

MWENYEKITI WA BARAZA LA WAZEE CHADEMA KYELA AFARIKI DUNIA

Mamia ya Wananchi wa Kyela - Mbeya tarehe 12 Machi, 2017 walikusanyika katika mazishi ya Antony R. Mapunda -Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa CHADEMA Kyela na Mwenyekiti wa Kitongoji cha Butiama kilichopo Kata ya Mbugani katika Mamlaka ya Mji wa Kyela.

Marehemu ambaye kipindi cha uhai wake alisifika kwa uongozi uliotukuka na msimamo wake thabiti kwenye mambo mbalimbali ya uongozi na utendaji, alikuwa ni mmoja wa waasisi wa Mageuzi nchini mwetu na kiongozi mahiri wa CHADEMA wilayani Kyela na pia wakati wa uhai wake Marehemu aliwahi kuwa Mchungaji wa Kanisa la T.A.G.

Msiba huo ambao ulihudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa CHADEMA akiwemo Mwenyekiti wa CHADEMA Wilaya ya Kyela ambaye pia ni Mwanasiasa mkongwe Alipipi Kasyupa ambaye alitumia msiba huo kuiasa jamii kuiga mfano wa maisha ya Mzee Mapunda haswa kwenye suala zima la uchapakazi, msimamo na ujasiri wa kuitetea jamii katika kero mbalimbali.


No comments:

Post a Comment