Thursday, February 2, 2017

SWALI LA MHESHIMIWA FREEMAN MBOWE KWA WAZIRI MKUUKufuatia Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kukataa kuwa si kweli rais Magufuli amepanga kuufuta upinzani nchini ifikapo mwaka 2020.

Kiongozi wa Kambi rasmi ya Upinzani Bungeni, Freeman Aikaeli Mbowe alimuuliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kama atakuwa tayari kuwajibika endapo kambi hiyo italeta uthibitisho ndani ya Bunge kuwa Rais na Serikali ya awamu ya 5 imepanga kuufuta Upinzani nchini ifakapo mwaka 2020.

Aidha Naibu Spika Dkt Tulia Akson Mwansasu alilikataa swali hilo kwakuwa sio swali la kisera hali iliyosababisha kambi rasmi ya upinzani kupiga mayowe kuonyesha kutokuunga mkono maelezo hayo ya Naibu Spika.

No comments:

Post a Comment