Thursday, February 9, 2017

HATIMAYE TUNDU LISSU APATA DHAMANA


Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu amefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa tuhuma za kutoa lugha ya kichochezi

Serikali imeleta hati ya kiapo ambayo inazuia Mh. Tundu Lissu asipewe dhamana.

Kibatala ambaye ni Wakili wa mtuhumiwa amepinga kuwa hicho kiapo kilicholetwa hakina mantiki yoyote kisheria kwa sababu kimeletwa kwa kuvizivizia. Halafu kina makosa mengi, kinazungumzia kuhusu kesi nyingine ambazo amewahi kutuhumiwa nazo, ambazo hazina uhusuiano na kesi ya leo. Kiapo hakitaji kimewahi kutolewa mbele ya Mwanasheria gani, kimepigwa muhuri tu.

Kibatala amelalamika kwamba uwepo wa kesi zingine hata kama zingekuwa mia moja (100) bado haziwezi kuzuia mtuhumiwa kupewa dhamana.

Kiapo kilichotolewa na serikali hakionyeshi ni katika Sheria ipi ambazo zinahusiana na hii kesi ili huyu mtuhumiwa asipewe dhamana.

Wamezungumzia kwamba mtuhumiwa asipewe dhamana kwa sababu ya usalama wake lakini wakashindwa kueleza tangu mwezi wa Januari 2017 alipofanya kosa analotuhumiwa, muda ambao sasa mwezi mzima alikuwa anaishije na labda kama amewahi kutoa taarifa kituo chochote cha Polisi au kwenye vyombo vyovyote vya dola kuwa anatishiwa usalama wake izingatiwe pia Lissu ni Mbunge. Hawajaeleza popote kwamba usalama wa Lissu unatishiwa kwa namna gani mathalani amewahi kukosowa na risasi wapi na wapi.

Wakili Kisenyi (tumefanikiwa kupatikana jina moja kwa sasa) ambaye ni mmoja wa jopo la Mawakili wa Serikali linaloundwa na Mawakili wane (4), ameomba dakika 20 ili akapitie vitabu vya Sheria kuangalia makosa yaliyotajwa kuwemo kwenye kiapo chake.

Hakimu amekataa na kuwaeleza Mawakili wa Serikali kuwa ndiyo maana mlikuja wanne na kuongeza kuwa pamoja na kwamba mliwapatia wenzenu kiapo hapa hapa lakini wao wamejibu kwa hoja nyingi.

Hakimu ameonekana kutokuwa mnyonge na kutoa dakika 10 tu.

Kesi itaendelea baada ya muda huo ili hakimu atolee maamuzi na ifahamike kama Lissu atapewa dhamana au lah!




-----Update: 2

Wakili wa Serikali, ndugu Kisenyi amekuja kujibu hoja zilizowasilishwa na upande wa utetezi kuhusu hati ya kiapo.

Wakili Kisenyi anasema Mahakama isiangalie makosa yaliyopo katika hati ya kiapo iliyowasilishwa na Mawakili wa Serikali.

Anasema mahakama ijiridhishe na mhuri uliopo kwenye kiapo na isihangaike kuangalia kiliapwa kwenye ofisi gani maana mhuri unaonyesha umegongwa na Wakili aliyopo Dar es Salaam.

Na kuhusu hoja kwamba hakuna facts zinazonyesha kuwa Askari anayemtuhumu Mh. Lissu amepata wapi habari za mtuhumiwa, Wakili Kisenyi amejibu kwamba Askari amezipata kwa njia za Kiintelijensia kwa kuwa yeye Mpelelezi.

Juu ya hoja ya usalama wa mtuhumiwa, Mawakili wa Serikali wamesema kuwa si lazima uwe usalama mtuhumiwa mwenyewe maana maneno anayoweza kutoa akiwa nje ya mahakama au Polisi yanaweza kusababisha uvunjivu wa Amani kwenye jumuiya nzima na jamii nzima ikahathirika hata kama si yeye pekee.

Kwa hiyo wameweka msisitizo kuwa kiapo kipo sawa.

Baada ya kuwasilisha majibu ya hoja, Mawakili wa Serikali wameiomba Mahakama ikubaliane na hati ya kiapo na hivyo imnyime Mh. Lissu dhamana.

Kesi imeharishwa tena kwa nusu saa. Hakimu atarejea baada ya muda huo kuja kutoa huku

-----Update: 3

Dhamana ya Mh. Tundu Lissu ipo wazi!

Maamuzi juu ya hukumu kama yalivyotolewa na Hakimu.

Vifungu vyote vilivyotumiwa na Mawakili wa Serikali kuzuia dhamana havikukidhi mahitaji ya kisheria na hivyo si miongoni mwa sababu zinazoweza kuzuia dhamana
Kuhusu masuala ya usalama wa mtuhumiwa, Hakimu kasema hakuna taarifa zozote za kina zilizotajwa kwenye kiapo kuthibitisha kuwa mtuhumiwa au jamii inaweza kuhatarika
Kiapo kilichowasilishwa na upande wa Serikali kimekuwa na mapungufu mengi, kimekosesewakosewa kimaandishi na hakikuwa na namba ya kesi wala hakikuonyesha kimechukiliwa wapi
Kufuatia maelezo hayo, Hakimu amehitimisha kwa kusema Mh. Tundu Lissu anaruhusiwa kudhaminiwa.

Patrick J. Assenga amejitokeza kumdhamini kwa dhamana ya TZS 20,000,000/= (milioni ishirini).

Kesi itaendelea tena tarehe 06/03/2017
Hali nje ya mahakama ilikuwa ya ulinzi mkali. Askari wenye silaha walikuwa wametanda. Haikuweza kufahamika haraka walikuwa na lengo gani. Lakini dalili zilionyesha walitaka Mh. Lissu aingie mikononi mwao akitoka nje ya mahakama. Vijana wa CHADEMA wameweza kuwachezashere askari na kutoweka na Mh. Lissu kuelekea kusiko julikana.

No comments:

Post a Comment