Monday, January 23, 2017

YALIYOJIRI KWENYE MKUTANO MKUU MAALUM WA CHADEMA KANDA YA SERENGETI SHINYANGA

Ijumaa Januari 20,2017 kumefanyika mkutano mkuu maalumu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Kanda ya Serengeti inayojumuisha mikoa ya Shinyanga,Mara na Simiyu umefanyika katika ukumbi wa mikutano Karena Hotel Mjini Shinyanga.

Viongozi mbalimbali wa kitaifa wa CHADEMA wamehudhuria mkutano huo ambao umeenda sambamba na kufanya uchaguzi wa viongozi wa kanda ya Serengeti ambapo John Heche amechaguliwa kuwa mwenyekiti,Gimbi Masaba kuwa makamu mwenyekiti n Catherine Ruge kuwa mweka hazina.

Mwenyekiti wa CHADEMA taifa Freeman Mbowe ametumia mkutano hiyo kutoa ujumbe kwa taifa kupitia vyombo vya habari.

Mbowe amesema nchi ya Tanzania inapitia changamoto nyingi kwa kipindi hiki lakini kubwa zaidi kuliko yote ni hofu inayotamalaki ndani ya taifa kwamba watu wameanza kujiona kuwa hawako salama sana ndani ya nchi yao.

Amesema kuna watu ambao wana hofu ya njaa,hofu ya kuporomoka kwa uchumi,hofu za kiusalama,lakini CHADEMA ina hofu kubwa kuhusu usalama wa viongozi wake,hofu kubwa kuhusu kutokutendewa haki viongozi wa cha hicho kuanzia viongozi wa kitaifa,kwenda kwa wabunge,madiwani,wenyeviti wa vijiji,wenyeviti wa mitaa hata na vitongoji pamoja na wanachama wao.

“Badala ya kujengwa hofu ni lazima sasa tusimamie imara kuijenga CHADEMA yenye nguvu kujenga upinzani wenye nguvu,kusimama kwa haki bila kuogopa”,amesema Mbowe.

“Ni juzi tu rais amemteua wabunge wengine katika orodha ya wabunge 10 anaoweza kuwateua,katiba ya nchi inasema anapaswa ateue 10,lakini kati yao wasipungue wanawake watano,lakini hadi jana rais ameshateua wabunge nane kati yao sita ni wanaume kwa maana hiyo tayari ameshavunja katiba”,anasema Mbowe.No comments:

Post a Comment