Selemani Methew Lowongo (Kushoto) Akipokea Kadi ya Uanachama alipojiunga na Chama cha Chadema.
Kosa walilokuwa wanatuhumiwa nalo ni kufanya mkutano bila kibali. Hukumu imetolewa leo 18.01.2017 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Lindi. Walioshitakiwa walikuwa sita lakini wanne wameachiwa huru.
Kwa mujibu wa Afisa Habari wa CHADEMA, Tumaini Makene amedai kuwa hukumu hii inaonekana ni ya kimkakati kwakuwa Mwenyekiti wa Chadema mkoa wa Lindi alikuwa ni mmoja ya wagombea wa Ubunge katika jimbo la Mtama jimbo aliloshinda Nape Nnauye (Ambaye ni Waziri wa Habari).
Pia Mwenyekiti huyo alikamatwa siku ambayo Mbunge wa Kawe na Mwenyekiti wa Baraza ya wanawake CHADEMA(BAWACHA), Halima Mdee lakini hakukuwa na mkutano wa siasa.
Aidha wanasheria wa CHADEMA wanaangalia uwezekano wa kukata rufaa dhidi ya hukumu hiyo.
No comments:
Post a Comment