Friday, October 14, 2016

Mbowe awaonya vikali wakuu wa mikoa na wilaya Nchini

Mwenyekiti wa Chadema Taifa Freeman Mbowe amelaani vikali tabia ya wakuu wa wilaya na mikoa nchini kuingilia mamlaka zisizo zao.

Kiongozi huyo alikuwa alikuwa akizungumza na wanahabari mjini Arusha mara baada ya kuhudhuria kesi ya Rufaa ya aliyekuwa mbunge wa Longido Onesmo Ole Nangole.

Kiongozi huyo wa upinzani bungeni ameonya na kulaani tabia ya mkuu wa mkoa wa Arusha akishirikiana na wakuu wake wa wilaya kudhalilisha madiwani wa Chadema bila sababu.

Mwenyekiti huyo amesema viongozi hao wa kuteuliwa wamekuwa wakitengua maamuzi ya vikao halali vya mabaraza vya madiwani kihuni na bila sababu za msingi ati kwa vile tu mabaraza hayo yanaongozwa na Chadema.
Mwenyekiti huyo amesema posho ambazo zinalipwa madiwani zilipitishwa na Baraza la madiwani wa CCM wakitaka kubadilisha posho hizo Mkuregenzi wa Jiji la Arusha anatakiwa kuwapatia madiwani waraka unatakiwa kutoka ofisi ya Tamisemi.

Kiongozi huyo mkuu wa upinzani nchini ameagiza wanasheria wa chama kuchukua hatua mara moja dhidi ya wakuu wa mikoa na wilaya wanaofanya vitendo vinavyokiuka maadili ya kazi zao.



No comments:

Post a Comment