Thursday, September 29, 2016

CHADEMA KUFANYA MKUTANO NA WAANDISHI WA HABARI IJUMAA TAREHE 30 SEPTEMBA 2016

Salaam

Waandishi wa vyombo mbalimbali vya habari leo wametutafuta wakitaka kujua au kupata taarifa kutoka CHADEMA juu ya mambo mawili.

1. Evergreen story na updates (rasmi) kuhusu Operesheni UKUTA na hatima siku ya maandamano na mikutano nchi nzima iliyotangazwa na chama.

2. Maoni au mtizamo wa CHADEMA kuhusu Ripoti ya Utafiti wa Taasisi ya Twaweza iliyotolewa leo juu ya maoni ya watu kuhusu UKUTA;

Naomba kutumia taarifa hii fupi kukitaarifu na kualika chombo chako kwenye press conference itakayofanyika kesho Ijumaa, Septemba 30, 2016, saa 5.00 asubuhi, ambapo mzungumzaji mkuu atakuwa ni Mwenyekiti wa Chama Taifa, akitoa tamko la chama kuhusu hatima ya maandamano na mikutano ya kisiasa nchi nzima yaliyopangwa na CHADEMA na masuala mengineyo yanayoendelea nchini.

Makene

Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano
CHADEMA

No comments:

Post a Comment