Saturday, July 30, 2016

CHADEMA NYANDA ZA JUU KUSINI NA NYASA WASEMA WAPO TAYARI KWA OPARESHENI UKUTA

Frank Mwaisumbe

CHAMA cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA) Kanda ya Nyanda za Juu Kusini (Nyasa) wameunga mkono maazimio yote yaliyotolewa na kamati kuu cha Chadema chini ya mwenyekiti wake Taifa Bw Freeman Mbowe ya kuazisha oparesheni UKUTA .
Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari leo na mwenyekiti wa kanda ya nyanda
za juu kusini Bw Frank Mwaisumbe alisema wamepokea kwa mikono miwili maamizimio hayo ya kuanzisha oparesheni UKUTA nchini nzima na kuwa wapo tayari kwa kushiriki .

“Kwa ujumla wake (Mkoa wa Mbeya, Songwe, Rukwa, Iringa na Njombe) inaunga mkono maazimio ya Kamati kuu ya Chama Chetu iliyoketi tarehe 27/07/2016 ya kupinga vikali aina zote za udikteta zinazoendelea na kufanywa na serikali ya chama cha Mapinduzi (CCM)….. na kuwa tupo tayari kuona Demokrasia
ya vyama vingi nchini Tanzania inaendelea kuimarika kama iliyo asisiwa na Baba wa Taifa Mwal. Julius kamabarage Nyerere, ambayo aliiacha ikiwa na amani na utulivu na kuwa nchi yenye kuruhusu mfumo wa vyama vingi”

Alisema kuwa kwa kuwa Tanzania ni moja kati ya nchi zinazoendeshwa kwa mfumo wa vyama vingi ni vema chama tawala CCM kuacha kufinyanga Demokrasia hiyo na kuviacha vyama vyote kufanya kazi ya kujiimarisha kwa uhuru na amani badala ya kuzuia vyama kuendesha mambo yao .

Kwani alisema ili chama kiwe imara na chenye nguvu ya kuleta ushindani ni lazima kuwekeza kwa wananchi na hivyo kuanzishwa kwa oparesheni UKUTA kutasaidia Chama chao kuwekeza kwa wananchi kazi ambayo hata CCM wamekuwa wakiendelea kuifanya hadi sasa .

Mwaisumbe alisemutakuwa ni uonevu mkubwa iwapo serikali ya CCM itazuia Chadema kuendelea na Oparesheni UKUTA wakati juzi Dodoma katika Uwanja wa Jamhuri aliyekuwa mwenyekiti wa CCM Taifa Rais Mstaafu Dr Jakaya Kikwete alifanya mkutano mkubwa ambao kimsingi si mkutano wa kiserikali ila ulikuwa ni mkutano wa Chama.

Alisema siasa safi ni pamoja na kuruhusu vyama vyote kuendelea ujenga vyama vyao ikiwa ni pamoja na kutawaliwa na uhuru wa kuongea na uhuru wa kukosoa bila kuvunja katiba ya nchi.

Bw Mwaisumbe alisema wao kama Chadema kanda ya Nyasa watahakikisha wanafanya zoezi hilo la Oparesheni UKUTA pasipo kuvuruga amani ya nchi na kuona mikutano yao yote inafanyika kwa uhuru na amani na wapo tayari kuendelea kulinda amani na utulivu.

“ sisi CHADEMA kanda ya Nyasa kwa pamoja tunajiunga na UKUTA Umoja wa Kupinga Udikteta Tanzania.. wa UKAWA na tupo tayari wakati wote kupambana na mtu yeyote anayevunja katiba na kuweka udikteta…. hii ni nchi yetu sote na tupewe uhuru kwa usawa bila kuvunja katiba ya nchi”


No comments:

Post a Comment