Monday, June 20, 2016

Kitendo kilichofanywa na polisi Dodoma na Kilimanjaro hatutakivumilia tena

TAMKO LA BARAZA LA VIJANA WA CHADEMA (BAVICHA) KULAANI VITENDO VYA UNYANYASAJI VINAVYOFANYWA NA JESHI LA POLISI


Baraza la Vijana wa Chadema ( BAVICHA) tunalaani vikali kitendo cha jeshi la Polisi kuvamia Mahafali ya CHASO mkoa wa Dodoma na Kilimanjaro kuzuia isifanyike.

Vitendo hivyo ni vya kihuni na havina ubinadamu wala havikufuata misingi ya Kidemokrasia na Utawala bora.Wakati Polisi wakifanya hivyo kwa CHADEMA huku ccm wanafanya mahafali zao na wanalindwa na jeshi la polisi,Ujinga huu sasa umefika mwisho.

Polisi wamevamia Mahafali ya vijana wetu na kuizuia kwa kuwa eti hakukuwa na kibali cha Mahafali, tumewauliza Polisi ni sheria gani inasema mtu akifanya Mahafali lazima aombe kibali cha Mahafali kwa la Polisi??

Polisi Dodoma walishindwa kujua hata wao kwanini wanazuia Mahafali,wakijichanganya eti kuna ugonjwa na mwisho wake wakasema maelekezo kutoka juu,hivi huyo alie juu ninani?,alichaguliwa nanani?? Anaishi wapi??

Polisi wamejivika majukumu yasio wahusu nakujifanya wao ni viranja wa ccm ,haisaidii kuendelea kutunyanyasa wakafikiri kuwa wanatufundisha uoga ,bali sasa wanatupa ujasiri wa kutafuta namna ya kuitafuta haki yetu ya msingi na wasitegee wakiivuruga nchi hii wataweza kuirudisha kama awali.

Nchi hii inapo kwenda ni kubaya sana,na sisi kama vijana hatutakubali kuona watu wachache wanataka kuharibu amani ya nchi kwa kukandamiza Demokrasia jambo ambalo ndio hasa litaanzisha machafuko halafu tukawanyamazia.

Tukiyaacha haya yaendelee katika nchi yetu,nikukubali zama za utumwa kurudi upya kwa njia nyingine kupitia Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na ccm kwa kutumia jeshi la Polisi ambalo muda wote limekuwa likiteleza maagizo haramu ya watawala.

Kuanzia Leo hatutakubali kupokea amri yeyote ya jeshi la Polisi yenye misingi ya kukandamiza Demokrasia ya nchi yetu kwakuwa tumepoteza imani na namna ambavyo jeshi la Polisi limekuwa likitekeleza majukumu wajibu wake kwa kutofuata utaratibu.

Tunapenda kuliambia jeshi la Polisi Kiwango cha uvumilivu kwetu kama vijana kinaelekea kufika mwisho na sasa tutaanza kuchukua hatua ya kupinga dhulumu,uonevu na ukandamizaji unaofanywa na jeshi la Polisi nchini kwa maelekezo ya Watawala.

Hatutachokaza mtu ,tutafuata utaratibu wa Kikatiba na hatutakubali kuvunja sheria ila hatutakubali kuona tena tunaendelea kunyanyaswa na jeshi la Polisi pamoja na watawala.

Mmetuzuia tusifanye mikutano tumekubali,mmetuzuia vikao vyetu vya ndani tumekubali,mmetuzuia kukaa vijiweni na wananchi wetu tumekubali sasa hata Mahafali zetu mnazuia??

Nafikiri umefika wakati wakuwaonesha Watanzania ninani anaevuruga amani ya nchi hii,hatutaa kimya tena .

Jiandaeni kutupiga,kwakuwa mna nguvu za kutupiga,jiandaeni kutufunga kwakuwa mnazo magereza za kutosha,jiandaeni kutupiga risasi na mabomu na maji ya kuwasha kwakuwa nyie ni jeshi lenye nguvu kuliko yote duniani.

Kumbukeni hakuna silaha yeyote wala jeshi lolote lililowahi kuishinda nguvu ya Umma,Polisi mnaipeleke nchi kubaya kusiko julikana.

Imetolewa June 19

BAVICHA Taifa

No comments:

Post a Comment