Mwita Waitara, Mbunge wa Jimbo la Ukonga, imeitaka serikali kuhakikisha inaweka huduma ya vituo vya polisi katika jimbo hilo jijini Dar es Salaam ili kukabiliana na matukio ya uhalifu yaliyoshamiri, anaandika Pendo Omary.
Akizungumza na MwanaHALISI Online jana Jijini Dar es Salaam, Waitara amesema “ jimbo zima la Ukonga hakuna kituo kikubwa cha polisi hata kimoja. Kwa sasa tunatumia kituo cha Stakishari kilichopo jimbo la Segerea. Hata vituo vidogo vilivyopo vinafugwa saa 12:00 jioni”.
Waitara amesema kituo cha Stakishari ambacho wanakitumia kwa sasa, uwezo wake wa kuhudumia majimbo mawili ni mdogo. Hasa kutokana na kutokuwa na usafiri wa uhakika pindi askari wa kituo hicho wanapohitajika kutoa huduma katika majimbo hayo.
“Askari wa Kituo cha Stakishari wanalazimika kutumia gari ya OCD. Inapotokea OCD kaondoka na gari, basi huduma ya polisi inayotumia gariinakosekana,” amesema Waitara.
Aidha, Waitara amelitaja tukio la Disema, mwaka jana la uvamizi, uporaji wa fedha na mauaji ya askari wawili kwenye Benki ya CRDB Tawi la Chanika kama moja ya matukio ya kiharijfu yanayochangiwa na kutokuwepo vituo vya polisi katika jimbo hilo.
“Mara baada ya kupata nafisi ya kuongoza jimbo hili tayari nimeshirikiana na wananchi. Tumeanza mchakato wa ujenzi wa vituo vikubwa vya polisi vitatu ambavyo vitakuwa kata za; Kivule, Msongora na kata ya Zingiziwa. Tunaiomba serikali na Jeshi la Polisi ituonge mkuno katika kutatua tatizo hili.” amesema Waitara.
No comments:
Post a Comment