Mdee aliyasema hayo jana katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Viwanja vya Sokoni Jimbo la Mtama Mkoani Lindi na kuhudhuriwa na wananchi wa Jimbo hilo.
"Juz Rais anasema eti mshahara wake 9.5 Millioni sasa atutajia Posho za kila siku ili kila Mtanzania ajue kiasi ambacho Rais anakipata na sio kudanganya wananchi,"alisema Mdee.
Mdee aliongeza kuwa wabunge wanalipwa mshahara Million3 lkn kuna posho mbali mbali kutokana na kuhudumia wananchi.
" Sisi wabunge mshahara wetu katika salary sleep unasoma Sh 3 Millioni lakini Posho na pesa ya mambo ya utendaji ya mbunge inafika 10 Millioni sasa Rais atuambie na yeye poshozake ni kiasi gani,"alisema Mdee.
Naye Mbunge wa Jimbo la Ndanda lililopoa Wilaya ya Masas Mkoani Mtwara Cecil Mwambe alisema kuwa wananchi wa Jimbo la Mtama wamekosa muwakilishi wa kuwasemea matatizo yao hasa ya upande wa kilimo cha korosho kutokana na Mbunge aliyepo Nape Nnauye hawez kusimama Bungeni na kuisema Serikali.
"Mtama mmekosa mwakilishi hapa kuna tatizo la korosho na mbunge aliyepo anashindwa kulisemea hivyo mtabaki hivyo hivyo bila kutatua tatizo lenu kwa kipindi cha Miaka Mitano,"alisema Mwambe
Hata hivyo mwenyekiti wa Bawacha anafanya ziara katika majimbo ya Lindi na Mtwara kwa kufungua matawi ya Chadema pomoja na kuongea na wanawake wa chama hicho.
No comments:
Post a Comment