Thursday, April 21, 2016

FOLENI, MAFURIKO KUWA HISTORIA HALMASHAURI YA MANISPAA YA KINONDONI.

Hayo yamesemwa leo Jumatano tarehe 20 Aprili 2016 na Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni Mh. Boniface Jackob wakati wa hafla ya kusaini Mkataba Na Kampuni ya MS/H.P GAUFF INGENIEURE GMBH&CO, KG -JBB ambayo ni mtaalam Mwelekezi (Consultant) atakayetoa Huduma za ushauri elekezi (Consultant services) katika, usimamizi wa ujenzi wa Miradi ya DMDP (Dar es salaam, Metropolitan, Development Project) itakayotekelezwa ndani ndani ya Manispaa ya Kinondoni wenye thamani ya URO 4.678580 Na USD 402833 utakaodumu hadi mwisho wa muda wa utekelezaji wa miradi hiyo.

Mtaalam huyu mwelekezi atakuwa Na jukumu la kuhakikisha kazi zitakazofanyika zinakuwa katika mpangilio uliokubalika, (Designing) Na kwa kuzingatia ubora Na thamani ya miradi (Value for Money) ili wananchi wote wa Manispaa ya Kinondoni Na jiji la Dar es salaam, wanufaike Na miradi hiyo kama ilivyokusudiwa katika malengo yake.

Halmashauri ya Kinondoni ina miradi 11 inayogusa maeneo ya Ujenzi wa Barabara za Halmashauri kwa kiwango cha lami zinazolenga kupunguza msongamano (Local Roads) Uboreshaji wa Miundombinu katika maeneo yasiyopangwa (Infrastructural upgrading in unplanned Settlements) Ujenzi wa mifereji ya maji ya mvua (Storm water drainage) Uimarishaji wa mifumo ya Mapato ya utawala Bora ya taasisi (Institutional Strengthen) Na Usimamizi wa taka ngumu (Solid waste Management)

Kwa mujibu wa upembuzi yakinifu uliofanywa Na wataalamu waelekezi (Consultants), Kati ya miradi yote 11 ya awamu ya kwanza na awamu ya pili, miradi 5 ya Barabara itakayotekelezwa katika awamu ya kwanza wakati wowote kuanzia sasa ambayo haihitaji ulipaji wa fidia katika utekelezaji na barabara 6 zitajengwa baada ya Manispaa kulipa fidia katika maeneo ya miradi, zote kwa ujumla zina urefu wa Kilometa 20.75 Na zitagharimu Tsh 26,552,114/= na fidia ya Tsh 6,672,251,760/=.

Mradi wa Uboreshaji wa maeneo yasiyopangwa utagusa kata 3 za Mburahati, Tandale Na Mwananyamala utakaohusisha uwekaji wa Huduma muhimu kwa kuboresha Miundombinu ya barabara, taa za barabarani, taka ngumu, njia za waenda kwa miguu Na maji safi utakaogharimu Tsh 1,264,576/= na fidia ya Tsh 180,413,275/=.

Aidha mradi wa Ujenzi wa mto Sinza (Mto Ng'ombe) wenye urefu wa Kilometa 7 kuanzia chuo cha maji Dar es salaam hadi mto Msimbazi kupitia kata 6 za Ubungo, Sinza, Mwananyamala, Ndugumbi, Magomeni na Hananasif umelenga kuuwezesha mto huo kupitisha maji kwa urahisi Na kuepusha mafuriko Na utagharimu Tsh 20,100,000/= Na utahitaji fidia ya Tsh 4,054,499,410/=.

Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni Mhe. Boniface Jacob amewahakikishia wananchi wote wa Manispaa ya Kinondoni kuwa kwa kushirikiana Na Baraza lake la Madiwani na Serikali kuu na wadau wengine wakiwemo waheshimiwa wabunge, watafanya kila jitihada ya kutafuta fedha za kulipia fidia ili miradi hiyo ambayo inahitaji fidia ianze kutekelezwa na kukamilika kwa wakati ili kuwapunguzia wananchi kero ya msongamano uliopo ndani ya jiji la Dar es salaam.



No comments:

Post a Comment