Saturday, February 6, 2016

MHESHIMIWA EDWARD LOWASSA AFANYA MKUTANO NA WAZEE WA CHADEMA

Aliyekuwa mgombea wa nafasi ya urais akiungwa mkono na vyama vinavyounda umoja wa katiba ya wananch UKAWA, Mh. Edward Lowassa amesema ni vema serikali ikahakikisha inapata suluhu ya mgogoro wa kisiasa visiwani Zanzibar kabla ya kufanyika kwa uchaguzi wa marudio machi 20 mwaka huu.

Mh. Edward Lowassa amesema hayo ofisini kwake Mikocheni jijini Dar es Salaam wakati wa kikao chake na wazee kutoka chama cha Chadema ambapo amesema anaunga mkono uongozi wa CUF kutokushiriki uchaguzi huo huku akisisitiza endapo serikali ikishindwa kumaliza mgogoro huo kabla ya mach 20 huenda hali ya kisiasa Zanzibar ikabadilika.

Aidha amewahakikishia wazee hao kuwa yeye na uongozi mzima wa UKAWA wako imara katika kuhakikisha wanatetea maslahi ya watanzania ambapo pia amemshukuru waziri mkuu kwa kuruhusu mikutano suala ambalo linawapa fursa ya kujipanga ili kuwashukuru watanzania waliojitokeza kupiga kura mapema 25.

Kwa mujibu wa risala ya wazee hao iliyosomwa na mzee Enock Ngombare, wamempongeza Mh. Lowassa kwa uvumilivu wake baada ya uchaguzi ambapo pia wamemhakikishia kuwa wako pamoja nae katika safari ya kuelekea mwaka 2020.

Aidha, aliwaomba wazee hao kutokata tamaa kwani kuna mambo mengi ya kufanya hadi kufikia malengo waliyojiwekea.

"Hali ya chama chetu na UKAWA iko vizuri, uchaguzi tulishinda, sisi tunajua, Jumuiya za Kimataifa zinajua na hata CCM wenyewe wanajua kama tulishinda, ila ubabe wao na dhuulma ndio wamefanya waliyofanya," alisema.

Lowassa alifafanua zaidi kuwa kama chama kinachojiandaa kushika dola hawakuwa tayari kuingia Ikulu kwa damu ya watanzania na ndiyo maana hata vijana walipomtaka atoe kauli ya kuingia barabarani anasema, "niliwazuia."

Katika mkutano huo ambao uliohudhuliwa na kada wa siku nyingi Kingune Ngombare Mwiru, Mh Lowassa amewataka wazanzibar na watanzania kwa ujumla kuwa watulivu na kuhakikisha wanadumisha amani ya nchi hasa katika kipindi hiki ambacho viongozi wanaendelea na juhudi za kutafuta suluhu ya kisiasa visiwani Zanzibar.

No comments:

Post a Comment