Tuesday, January 12, 2016

SALAMU ZA RAMBIRAMBI KUFUATIA KIFO CHA ALIYEKUWA MBUNGE WA VITI MAALUM CHADEMA MHESHIMIWA LETICIA NYERERE


SALAMU ZA RAMBIRAMBI KUFUATIA KIFO CHA ALIYEKUWA MBUNGE WA VITI MAALUM CHADEMA 
MHESHIMIWA LETICIA NYERERE

Napenda kuchukua fursa hii kwa niaba ya Viongozi, wanachama na wapenzi wa Chadema wa Tawi la Washington DC, Marekani, kutuma salamu za pole kwa familia ya aliyekuwa Mbunge wa viti maalum Chadema Kupitia Jimbo la Kwimba Mheshimiwa Leticia Nyerere kilichotokea baada ya kuugua kwa muda mfupi hapa Maryland, Marekani, siku ya Jumapili Tarehe 10 Januari 2016. Kwa hakika tumepokea taarifa ya msiba wa mheshimiwa Leticia Nyerere kwa mshtuko mkubwa kutokana na kumbukumbu ya mchango mkubwa aliyotoa kwenye kufungua Tawi letu la Chadema hapa Washington DC, Marekani. Pia kwa mchango wake aliyotoa akiwa kama mbunge wa Viti Maalum kupitia Chadema. Kwa kweli bado tulikuwa tunahitaji sana mchango wake lakini mpango wa mungu hauna makosa.


Mungu ailaze roho ya Marehemu Leticia Nyerere mahali pema peponi, Amin.

Mwenyekiti wa chadema Washington DC, Marekani
Kalley Pandukizi

No comments:

Post a Comment