Hatimaye tumemaliza hatua muhimu ya vikao vya uchaguzi wa Mameya wa Ilala na Kinondoni.
Tumeshinda na tutaongoza Manispaa hizi baada ya mnyukano wa kihistoria kuziba kila mbinu ya CCM kuhujumu kwa kutugawa kupitia rushwa, vitisho na hata kupindisha sheria.
Imedhihirisha tena manufaa na nguvu ya Umoja wetu wa UKAWA. Asanteni sana viongozi na wapiganaji wetu katika ushirika huu.
Kwa taarifa, Manispaa hizi mbili kwa sasa zinakusanya zaidi ya shs 65 billion kila moja kwa mwaka.
Zikisimamiwa vizuri, zina uwezo akiba (potential) wa kukusanya zaidi ya shs billion 50 kila moja kwa mwezi.
Halmashauri nyingi nchini hukusanya wastani wa shs billioni moja kwa mwaka.
Tafsiri yake ni kuwa makusanyo ya Manispaa moja ya Dar ni sawa au zaidi ya Halmashauri zote nchini nje ya Dar!!
Ukweli huu unatufikirisha mengi hususan kuhusu uzalishaji na tofauti kubwa ya kimapato kati ya Dar na Mikoa na Wilaya zetu.
Ndiyo maana CCM imewawia vigumu kukubali kuliachia Jiji la Dar japo sera zao ndiyo zimezalisha tofauti hii ya kutisha ya kimapato katka Taifa letu.
Haya, tujipongeze kwa kiasi na tuingie kazini sasa kuonyesha tofauti chanya.
Nawatakia wote waliokabidhiwa dhamana hii utendaji wenye weledi, uaminifu, kujali na zaidi wenye kusimamia haki na ustawi kwa wote.
Freeman A. Mbowe
MKT CHADEMA & KUB
No comments:
Post a Comment