Monday, September 14, 2015

TASWIRA ZAIDI ZA ZIARA YA KAMPENI YA URAIS YA MHESHIMIWA EDWARD LOWASSA MKOANI SINGIDAMgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akihutubia Mkutano wa hadhara wa Kampeni, uliofanyika kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Ilongero, Jimbo la Singida Kaskazini, leo Septemba 13, 2015. katika hotuba yake, Mh. Lowassa amesema iwapo atapata ridhaa ya wananchi kuwa Rais wa Tanzania, ataanzisha viwanda vya kusindika zao la alizeti, ili wakulima wa zao hilo waweze kufaidika na pia atakabiliana na kero zote za Mkoa wa Singida kwa ujumla. Mh. Lowassa, kesho Septemba 14, 2015 ataendelea na ziara yake ya Kampeni katika Mkoa Shinyanga, baada ya leo kumaliza katika Mkoa wa Singinda, kwenye Majimbo ya Manyoni Magharibi, Singida Kaskazini, Iramba Mashariki na Iramba Magharibi.

Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akimnadi Mgombea Ubunge wa UKAWA kupitia CHADEMA katika Jimbo la Singida Kaskazini, David Djumbe, wakati wa Mkutano wake wa Kampeni, uliofanyika kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Ilongero, Jimbo la Singida Kaskazini, leo Septemba 13, 2015.


Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, baadhi ya wagombea wa Udiwani wa maeneo mbalimbali ya Jimbo la Singida Kaskazini, wakati wa Mkutano wake wa Kampeni, uliofanyika kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Ilongero, Jimbo la Singida Kaskazini, leo Septemba 13, 2015.
Wananchi wa Ilongero, Singida Kaskazini wakifatilia kwa makini hotuba ya Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa.
Picha kwa hisani ya Othman Michuzi

No comments:

Post a Comment