Sunday, August 23, 2015

UKAWA ZANZIBAR : MAALIM SEIF SHARIFF HAMAD ACHUKUA RASMI FOMU YA KUGOMBEA URAI WA ZANZIBAR

Mgombea Urais wa Zanzibar wa UKAWA kupitia Chama cha Wananchi CUF, Maalim Seif Sharif Hamad akionyesha mkoba wenye Fomu za kuwania nafasi hiyo, leo Agosti 23, 2015, kwenye Ukumbi wa Salama, Bwawani, Zanzibar.
Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), Jecha Salim Jecha akimkabidhi Mgombea Urais wa Zanzibar wa UKAWA kupitia Chama cha Wananchi CUF, Maalim Seif Sharif Hamad, Fomu za kuwania nafasi hiyo, leo Agosti 23, 2015, kwenye Ukumbi wa Salama, Bwawani, Zanzibar.
Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa akimpongeza Mgombea Urais wa Zanzibar wa UKAWA kupitia Chama cha Wananchi CUF, Maalim Seif Sharif Hamad, baada ya kuchukua Fomu za kuwania nafasi hiyo, leo Agosti 23, 2015, kwenye Ukumbi wa Salama, Bwawani, Zanzibar
Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), Jecha Salim Jecha akisoma taarifa ya muongozo kwa Mgombea Urais wa Zanzibar wa UKAWA kupitia Chama cha Wananchi CUF, Maalim Seif Sharif Hamad, wakati wa kuchukua Fomu ya kuwania nafasi hiyo, leo Agosti 23, 2015, kwenye Ukumbi wa Salama, Bwawani, Zanzibar. Maalim Seif alisindikizwa na Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa,Mgombea Mweza, Dkt. Juma Haji Duni pamoja na viongozi wengine wanaounda UKAWA.
Mgombea Urais wa Zanzibar wa UKAWA kupitia Chama cha Wananchi CUF, Maalim Seif Sharif Hamad akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo Agosti 23, 2015, kwenye Ukumbi wa Salama, Bwawani, Zanzibar. Kulia kwake ni Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa pamoja na Mgombea Mweza wake, Dkt. Juma Haji Duni

No comments:

Post a Comment