Tuesday, August 18, 2015

Ofisi ya Chadema Morogoro Mjini Yavamiwa.

Na Bryceson Mathias, MorogoroOfisi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Morogoro Mjini, zimevamiwa na Viongozi wake kukimbia, baada ya kusikika Taarifa za kukatwa kwa Majina ya Washindi wa Kura za Maoni ya Uchaguzi wa Udiwani Kata za Morogoro, wakipinga Washindi wao kukatwa.

Dosari hiyo inayopelekea kukigawa Chadema na kukiingiza kwenye Mgogoro, imepingwa na Wanachama walioapa Watahakikisha wanakikomboa Chama kutoka kwenye Makucha ya baadhi ya Viongozi Mamluki, wanaodaiwa kutumiwa na Chama cha Mapinduzi (CCM) kukihujumu Chadema kwa Goli la Mkono.

Akizungumza na Mtandao huu, Kiongozi wa Kanda, Idd Kizota, ambaye muda wote alipoulizwa juu ya Mgogoro huo alikuwa Mkali kama Pilipili alisema, Mtu yeyote ambaye anaona ameonewa, akate Rufaa ngazi ya juu, lakini asikusanye watu na kufanya fujo.

Alipoulizwa kwa nini washindi wa Uchaguzi wamekatwa alidai, Kuna sababu mbalimbali ambazo hakutaja, na alipoambiwa kuwa Uongozi akiwemo yeye wanatuhumiwa kutumiwa na Chama cha Mapinduzi(CCM) waweke watu dhaifu kukiharibu Chadema ili kuandaa ‘Goli la Mkono’, alidai huo ni upuuzi.

“Kama Mtu anadhani ameonewa, anatakiwa kukata rufaa kwenye Vikao vya Juu. Wengi wawanaolalamika ni Wazuri kwenye Makaratasi, lakini wakienda kwa Wananchi wanashindwa……, ambapo alipoulizwa mbona wameshinda alikuwa Mkali na Kufoka, ‘Ujinga Sitaki hata angekuwa nani!”.alisema Kizota.

Wanachama wa Chadema waliohojiwa kwa nyakati tofauti wakitaka wasitajwe walisema, Chadema Taifa wanatakiwa kuuangalia upya Uongozi wa Chadema Kanda ya Kati na ule wa Morogoro na Wilaya ya Mvomero, ili iwekwe ‘Task Force’ kuelekea Uchaguzi Mkuu, kwa sababu hawana dhamira Njema na Chadema.

Kata zinazolalamikia Ushindi wa Matokeo ya Kura ya Maoni ya Udiwani na Washindi wao kukatwa ni pamoja na Kihonda Magorofani, Kirakala, Mazimbu, K/Ndege, Doma, Lukobe (Waliogomea Uchaguzi mpya), Uwanja wa Taifa, Chamwino ambao inadaiwa Wanalalamikia amewekwa Mgombea toka CCM asiyejua kusoma na kuandika ili tu, CCM ishinde kwa Urahisi.

Awali kilienezwa taarifa za Kwamba, Mgombea wa Ubunge jimbo la Mvomero, Matokeo Warden Mang’eta, amekatwa, ambapo Wana Chadema wa Jimbo hilo walitaka kuanza kutaka kufunga safari kuelekea Dumila Ofisi ya Wilaya na Kindumbwendubwe Chalia, lakini Kizota alikanusha kuwa Mgombea huo amekatwa, jambo ambalo Kadi za Chadema zilisalimika Kukuchomwa.

No comments:

Post a Comment